Home » » KAMPUNI YA UJENZI WA BARABARA YA KICHINA LAWAMANI KWA KUVAMIA ENEO LA SHULE

KAMPUNI YA UJENZI WA BARABARA YA KICHINA LAWAMANI KWA KUVAMIA ENEO LA SHULE


Na  Walter  Mguluchuma
Mpanda Katavi
Kampuni ya   China  Raiway  Seventh Rroup Ltd (YAKICHINA) inayojenga barabara kwa kiwango cha rami  ya kutoka Mpanda Mjini  Mkoani Katavi kuelekea Sitalike Wilaya ya Mlele  inalalamikiwa na  uongozi wa Kijiji na wananchi wa Kijiji cha  Magamba na kamati ya shule ya Msingi Magamba  kuwa imevamia  eneo la shule hiyo bila idhini na kufanya shughuli za uchimbaji wa changalawe
Malalamiko hayo yametolewa hapo jana kwenye kikao cha  kamati ya shule ya Msingi ya Magamba  na  uongozi wa kijiji hicho  waliokutana kwenye shule ya Msingi ya Magamba kwa lengo la kuijadili kampuni hiyo ya Kichina kwa kitendo  hicho cha kuvamia eneo hilo la shule
Kwenye kikao hicho wajumbe walimtaka Afisa Mtendaji wa Kijiji hicho George Ilesha  ambae pia ni Kaimu afisa Mtendaji wa Kata ya Magamba  atoe taarifa mbele ya kikao hicho ya kueleza ni kikao gani cha kamati ya shule  au uongozi wa kijiji uliwaruhusu kampuni hiyo kufanya shughuli kwenye eneo la shule
Afisa  Mtendaji huyo alieleza kuwa  yeye kama kiongozi wa Kijiji na Kata hiyo  hajahusika kwenye kikao chochote ambacho kilitowa maamuzi ya kuipatia eneo la shule  kampuni hiyo ya Kichina
 Alisema  siku mbili kabla  ya  kikao  alifuatwa na baadhi ya wananchi wa Kijiji hicho waliotaka awaeleze ni  kikao gani cha kamati ya  shule au  cha kijiji kilichotoka eneo la shule hiyo  kwa kampuni ya kichina
Ilesha alieleza  wanakijiji hao walidai kuwa wanazotaarifa kuwa  kuna viongozi wa kijiji hicho wameuza eneo hilo kwa kampuni hiyo ya kichina  na wanawafahamu
Kwaupande wake  mwalimu  Mkuu wa shule ya Msingi ya Magamba  Yohana Kasansa  alisema wao  kama uongozi wa shule walishitushwa kuona eneo lao limevamiwa  na kampuni hiyo ya ujenzi wa barabaea bila wao kuwa na taarifa yoyote ile
Alifafanua eneo hilo wamekuwa  wakilitumia  kwa ajili ya kilimo cha mahindi  ambayo huwasaidia wanafunzi kwa ajiri ya kupata chakula cha mchana
Kikao hicho kilimwagiza  Afisa mtendaji wa Kijiji kuiandikia barua  haraka iwezekanavyo kampuni hiyo ya Kichina  kuacha kufanya shughuli kwenye eneo hilo la shule ya Magamba  na atowe taarifa kwa jeshi la polisi
 Nae Meneja wa Tanroods Mkoa wa Katavi Mwandisi Izack Kamwelwe alisema  alipokea malalamiko kutoka kwa Diwani wa kata hiyo  Philipo Kalyalya  na alikwenda kwenye eneo hilo na kuiagiza kampuni hiyo kusimamisha shughuli kwenye eneo hilo mpaka hapo muafaka utakapo kuwa umepatikana
Alisema hata hivyo jana Meneja wa mradi wa kampuni hiyo ya kichina alikwenda ofisini kwake akiwa na nyaraka zinazoonyesha kampuni hiyo ilivyofuata taratibu na  kupewa eneo hilo kwa ajiri ya uchimbaji wa changalawe
 Alieleza  kampuni  hiyo inaonyesha  kwenye mkataba huo wameisha kilipa fedha kijiji hicho kwa ajiri ya kufanya shughuli zao hapo hata hivyo inaonyesha  kuna viongozi wa kijiji hicho wamechukua fedha kwa  manufaa yao binafsi
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa