Na Walter Mguluchuma
Katavi
Miradi mingi ya ujenzi wa Barabara za Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi zinashindwa kukamilika kwa wakati kutokana na wakandarasi wengi walioko Mkoani Katavi kutokuwa na mitambo ya kufanyia kazi
Hayo yamesemwa hivi karibuni na Mkugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda Stomihn Chang’ah wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda kilichofanyika hivi karibuni kwenye ukumbi wa idara ya maji mjini hapa
Chang’ah alitowa kauli hiyo kufuatia swali lililoulizwa kwenye kikao cha baraza hilo na Diwani wa Kata ya Kabungu Selemani Kasonso aliyetaka kujua sababu zinazosababisha miradi ya ujenzi wa barabara za Halmashauri hiyo kutokamilika kwa wakati
Mkurugenze wa Halmashauri hiyo alieleza baraza hilo la madiwani kuwa lipo tatizo la miradi ya ujenzi wa barabara kutokamilika kwa wakati kutokana na sababu mbalimbali
Alitaja sababu kubwa inayokwamisha miradi ya ujenzi wa barabara kwa wakati ni wakandasi wengi walioko katika Mkoa wa Katavi wanaokuwa wamepewa kazi ya uzabuni wengi wao wamekuwa hawana mitambo ya kufanyia kazi
Alisema hivyo wamekuwa wakitegemea kukodi mitambo kwa wakandarasi wengine ambapo wakati mwingine wenye mitambo hiyo na wao wamekuwa wakiwa na shughuli kwenye maeneo mengine Mkoani hapa na hari inawafanya washindwe kupata mitambo hiyo kwa wakati na kuwafanya kuanza kazi kwa muda wa kuchelewa
Chang’ah alileleza baraza hilo tayari wameisha anza kuwachukulia hatua baadhi ya wakandarasi ambao wameshindwa kumaliza miradi ya ujenzi wa barabara kwa wakati uliopangwa
Alisema Halmashauri inaandaa utaratibu wa kuwafutia mikataba wakandarasi wote ambao hawaja kamilisha miradi waliopewa kufanya
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment