Na Walter Mguluchuma
Mpanda Katavi
Wananchi wa Kijiji cha Mwese Tarafa ya Mwese Wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi wametishia kutomchagua Diwani wa Kata yao Juma Hawazi kwenye uchaguzi mkuu ujao wa mwakani endapo hawatakuwa wametengenezewa barabara
Hayo yalielezwa hivi kwenye kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri Ya Wilaya ya Mpanda kilichofanyika kwenye ukumbi wa Idara ya maji mjini Mpanda
Diwani wa viti maalumu wa Tarafa hiyo ya Mwese Thiodela Kisesa alilieleza Baraza hilo la madiwani kuwa hivi karibuni walifanya mkutano wa hadhara kwenye Kijiji cha Mwese ayeye akiwa na Diwani Juma Hawazi na walipata wakati mgumu kwenye mkutano huo
Diwani Kisesa alieleza wananchi hao walisema kwenyemkutano huo kuwa hawata kuwa tayari kumchagua Diwani Hawazi kwenye uchaguzi mkuu ujao wa mwakani endapo barabara ya kutoka kwenye kijiji hicho kuelekea kijiji wanachopakana nacho cha Kalya kilichopo Mkoani Kigoma endapo haitakuwa imetengenezwa
Alifafanua barabara hiyo ni ya muhimu sana kwa wananchi wa kijiji hicho kwani ndio inayo waunganisha wananchi wa vijiji hivyo viwili
Alisema ilikumusuru Diwani huyo kwenye uchaguzi mkuu wa ujao kwa wapiga kura wake Halmashauri ya Wilaya iangalie uwezekano wa kuitengeneza barabara hiyo
Alieleza matengenezo ya barabara hiyo siyo lazima yasubili fedha za kutoka kwa wafadhiri bali Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda iangalie uwezekano wa kutengeneza barabara hiyo kwa kutumia frdha za makusanyo ya mapato yake ya ndani
Kwa upande wake Afisa maendeleo na ustawi wa jamii wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda Jastine Tibenderana alisema Halmashauri hiyo ipo kwenye mpango wa kutengeneza barabara hiyo na inaendelea na mipango ya kupata wafadhili
0 comments:
Post a Comment