N a Walter Mguluchuma
Mpanda Katavi
Viongozi wa watano Chama cha CHADEMA wa Mkoa wa Katavi na wafuasi kumi na moja wa Chama hicho wamefikishwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya ya Mpanda kwa tuhuma za kufanya maandamano bila kibali
Watuhumiwa hao walifikishwa kizimbani hapo jana mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Mpanda Fransinci Nyando
Mwendesha mashitaka mkaguzi msaidizi wa polisi Nathaniel Silomba aliiambia Mahakama kuwa washitakiwa hao walitenda kosa hilo hapo Septemba 25 mwaka huu majira ya saa tano na nusu asubuhi katika eneo la mtaa wa Majengo A mjini Mpanda
Alidai mahakamani hapo kuwa siku hiyo ya tukio watuhumiwa walifanya maandamano yalioanzia kwenye ofisi za Chama chao yaliokuwa na lengo ya kushinikiza kusitishwa kwa Bunge maalumu la katiba huku wakiwa hawana kibali cha kuwaruhusu kufanya maandamano hayo
Viongozi waliofikishwa kizimbani ni Almasi Ibrahimu Ntije Katibu wa CHADEMA wa Mkoa wa Katavi Abrahma Mapunda Mwenyekiti wa Chadema wa Wilaya ya Mpanda Hamisa Korongo Mwenyeti wa Bawacha wa Mkoa Lamack Constantino katibu wa jimbo la Mpanda mjini na Fransisco Misigalo katibu wa Bavicha wa Mkoa
Washitakiwa wengine ni Seif Ntije , Emil Kalomo , Mwailwa James , Kasena Maulid ,Seleman Hamis , Mariamu Omari ,Kenedy Zakayo ,Shaban Ibrahimu, Cretus Aloyc na ,Mlokozi Bagasheki
Watuhumiwa hao wote kumi na sita wamepelekwa rumande baada ya kushindwa kutimiza mashariti ya mdhamana ambapo kila mshitakiwa alikuwa anatakiwa kuwa na wadhamini wawili walio na mali zisizo hamishika
Hakimu Mkazi Fransinci Nyando aliharisha kesi hiyo hadi Oktoba 8 mwaka huu itakapo tajwa tena kutokana na ombi la mwendesha mashitaka aliomba kutokana na upelelezi wa kesi hiyo kuwa bado unaendelea
0 comments:
Post a Comment