Friday, September 26, 2014

VINGOZI WA CHADEMA KIZIMBANI KWA KUFANYA MAANDAMANO BILA KIBALI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

  N a  Walter  Mguluchuma
Mpanda Katavi
  Viongozi wa watano   Chama cha   CHADEMA    wa  Mkoa wa Katavi na  wafuasi kumi na  moja  wa  Chama hicho wamefikishwa  kizimbani  katika Mahakama ya Wilaya ya Mpanda  kwa tuhuma za  kufanya maandamano bila kibali
 Watuhumiwa hao walifikishwa kizimbani hapo jana mbele ya Hakimu Mkazi  wa Mahakama  ya Wilaya ya Mpanda  Fransinci Nyando
Mwendesha mashitaka   mkaguzi msaidizi wa polisi  Nathaniel  Silomba  aliiambia Mahakama  kuwa washitakiwa  hao walitenda kosa hilo hapo Septemba  25  mwaka huu majira ya saa tano na nusu asubuhi  katika eneo la mtaa wa  Majengo A mjini  Mpanda
  Alidai mahakamani  hapo kuwa siku hiyo ya tukio watuhumiwa walifanya  maandamano  yalioanzia  kwenye ofisi za Chama chao yaliokuwa na lengo  ya kushinikiza  kusitishwa kwa Bunge maalumu la katiba huku wakiwa hawana kibali cha kuwaruhusu kufanya maandamano hayo
 Viongozi waliofikishwa kizimbani ni Almasi   Ibrahimu Ntije Katibu wa CHADEMA wa Mkoa wa  Katavi    Abrahma Mapunda  Mwenyekiti wa Chadema wa Wilaya ya Mpanda  Hamisa Korongo Mwenyeti wa  Bawacha wa Mkoa  Lamack  Constantino   katibu wa jimbo la Mpanda mjini na  Fransisco Misigalo katibu wa Bavicha wa Mkoa
 Washitakiwa wengine ni  Seif Ntije , Emil Kalomo , Mwailwa  James , Kasena Maulid ,Seleman Hamis , Mariamu Omari ,Kenedy   Zakayo ,Shaban Ibrahimu, Cretus  Aloyc na ,Mlokozi    Bagasheki
Watuhumiwa hao wote kumi na sita wamepelekwa rumande baada ya kushindwa kutimiza mashariti ya mdhamana ambapo kila mshitakiwa alikuwa anatakiwa kuwa na wadhamini wawili walio na mali zisizo hamishika

Hakimu Mkazi Fransinci Nyando aliharisha kesi hiyo hadi Oktoba  8  mwaka huu itakapo tajwa tena kutokana na ombi la mwendesha mashitaka  aliomba  kutokana na upelelezi wa kesi hiyo  kuwa bado unaendelea

No comments:

Post a Comment