Na Walter Mguluchuma
Katavi
Viongozi watatu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wa Mkoa wa Katavi na wafuasi 14 h wa chama hicho wanashikiliwa na jeshi la Polisi kwa tuhuma za kufanya maandamano bila kibali ya kuishinikiza Seerikali isitishe kikao cha Bunge maalumu ya Katiba
Viongozi hao wa Chadema wamekamatwa jana majira ya saa nne asubuhi kwenye eneo la zahanati ya Kasimba katika mtaa wa Majengo A wakati wakiwa wanaandamana kuelekea kwenye eneo la viwanja vya Mpanda Hotel ambako walikuwa wamepanga kufanya mkutano wa hadhara mara baada ya maandamano hayo
Viongozi wanaoshikiliwa na polisi ni Katibu wa Chadema wa Mkoa wa Katavi Almasi Ntije Mwenyekiti wa Chadema wa Wilaya ya Mpanda Abrahamu Mapunda na Katibu wa Chadema wa Jimbo la Mpanda Mjini Cretus Nkumba pamoja na wafuasi wao 14 na wengine walifanikiwa kutoroka
Awali viongozi wa Chama hicho waliandika barua hapo Septemba 22 kwa jeshi la polisi wakiomba kufanya maandamano tarehe 25 pamoja na mkutano wa hadhara kwenye viwanja vya Mpanda Hotel
Hata hivyo barua hiyo iliwezakujibiwa na jeshi la Polisi Wilaya ya Mpanda hapo Septemba 24 ikikitaka chama hicho kisifanye maandamano wala mkutano wa hadhara
Kwa mujibu Katibu wa Chadema wa Wilaya ya Mpanda idd Faraja alieleza kuwa Chama hicho kiliamua kufanya maandamano hayo baada ya kuwa wamefanya maandalizi ya maandamano hayo na jeshi la polisi kuchelewa kuwapatia barua ya kuwazuia kufanya maandamano na mkutano
Alisema kitendo cha polisi kuchelewa kujibu barua yao ya kuomba kibali walivyoona imekuwa kimya walijijua kuwa wamekubaliwa
Ofisi za Chadema ambazo zipo katika mtaa wa Majengo A jana kutwa nzima zimeshinda huku zikiwa zimezungukwa na Askari wa Jeshi la Polisi waliokuwa na silaha na hari ya ulinzi ya kituo kikuu cha Wilaya ya Mpanda kiliimalishwa baada ya kuzungukwa na askari polisi waliokuwa na silaha wakihofia kuvamiwa kwa kituo hicho na wafuasi wa Chaedema
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashari amethibitisha kukamatwa kwa viongozi hao wa Chadema na wafuasi wao na bado wanashikiliwa na jeshi hilo
No comments:
Post a Comment