Monday, September 29, 2014

WAKANDARASISI WA MKOA WA KATAVI WANASHINDWA KUMALIZA KAZI KUTOKANA NA KUTOKUWA NA MITAMBO


Na  Walter  Mguluchuma
Katavi
Miradi mingi ya ujenzi wa Barabara  za Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda Mkoa wa  Katavi zinashindwa kukamilika kwa wakati kutokana na wakandarasi wengi walioko Mkoani Katavi  kutokuwa na mitambo ya kufanyia kazi
Hayo yamesemwa hivi karibuni na  Mkugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda  Stomihn Chang’ah  wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda kilichofanyika hivi karibuni kwenye ukumbi wa idara ya maji mjini hapa
Chang’ah alitowa kauli hiyo kufuatia swali lililoulizwa kwenye kikao cha baraza hilo  na Diwani wa Kata ya Kabungu Selemani Kasonso  aliyetaka kujua sababu zinazosababisha miradi ya ujenzi wa barabara za Halmashauri hiyo  kutokamilika kwa wakati
Mkurugenze wa Halmashauri hiyo alieleza  baraza hilo la madiwani kuwa lipo tatizo la miradi ya ujenzi wa barabara kutokamilika kwa wakati kutokana na sababu mbalimbali
 Alitaja sababu kubwa inayokwamisha miradi ya ujenzi wa barabara kwa wakati ni  wakandasi wengi walioko katika Mkoa wa Katavi wanaokuwa wamepewa kazi ya uzabuni  wengi wao wamekuwa hawana mitambo ya kufanyia kazi
 Alisema  hivyo wamekuwa wakitegemea kukodi mitambo kwa wakandarasi wengine  ambapo  wakati mwingine wenye mitambo hiyo na wao wamekuwa wakiwa na shughuli kwenye maeneo mengine Mkoani hapa  na hari inawafanya washindwe kupata mitambo hiyo kwa wakati  na kuwafanya kuanza kazi kwa muda  wa kuchelewa
 Chang’ah alileleza  baraza hilo  tayari wameisha anza kuwachukulia hatua  baadhi ya wakandarasi ambao wameshindwa kumaliza miradi ya ujenzi wa barabara kwa wakati uliopangwa

 Alisema Halmashauri inaandaa utaratibu wa kuwafutia  mikataba wakandarasi wote  ambao hawaja  kamilisha  miradi  waliopewa kufanya
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

No comments:

Post a Comment