Na Walter
Mguluchuma
Mpanda Katavi
Kampuni ya China
Raiway Seventh Rroup Ltd
(YAKICHINA) inayojenga barabara kwa kiwango cha rami ya kutoka Mpanda Mjini Mkoani Katavi kuelekea Sitalike Wilaya ya
Mlele inalalamikiwa na uongozi wa Kijiji na wananchi wa Kijiji cha Magamba na kamati ya shule ya Msingi
Magamba kuwa imevamia eneo la shule hiyo bila idhini na kufanya
shughuli za uchimbaji wa changalawe
Malalamiko hayo
yametolewa hapo jana kwenye kikao cha
kamati ya shule ya Msingi ya Magamba
na uongozi wa kijiji hicho waliokutana kwenye shule ya Msingi ya Magamba
kwa lengo la kuijadili kampuni hiyo ya Kichina kwa kitendo hicho cha kuvamia eneo hilo la shule
Kwenye kikao
hicho wajumbe walimtaka Afisa Mtendaji wa Kijiji hicho George Ilesha ambae pia ni Kaimu afisa Mtendaji wa Kata ya
Magamba atoe taarifa mbele ya kikao
hicho ya kueleza ni kikao gani cha kamati ya shule au uongozi wa kijiji uliwaruhusu kampuni hiyo
kufanya shughuli kwenye eneo la shule
Afisa Mtendaji huyo alieleza kuwa yeye kama kiongozi wa Kijiji na Kata
hiyo hajahusika kwenye kikao chochote ambacho
kilitowa maamuzi ya kuipatia eneo la shule
kampuni hiyo ya Kichina
Alisema
siku mbili kabla ya kikao
alifuatwa na baadhi ya wananchi wa Kijiji hicho waliotaka awaeleze
ni kikao gani cha kamati ya shule au
cha kijiji kilichotoka eneo la shule hiyo kwa kampuni ya kichina
Ilesha
alieleza wanakijiji hao walidai kuwa
wanazotaarifa kuwa kuna viongozi wa
kijiji hicho wameuza eneo hilo kwa kampuni hiyo ya kichina na wanawafahamu
Kwaupande wake mwalimu
Mkuu wa shule ya Msingi ya Magamba Yohana Kasansa
alisema wao kama uongozi wa shule
walishitushwa kuona eneo lao limevamiwa
na kampuni hiyo ya ujenzi wa barabaea bila wao kuwa na taarifa yoyote
ile
Alifafanua eneo
hilo wamekuwa wakilitumia kwa ajili ya kilimo cha mahindi ambayo huwasaidia wanafunzi kwa ajiri ya
kupata chakula cha mchana
Kikao hicho
kilimwagiza Afisa mtendaji wa Kijiji
kuiandikia barua haraka iwezekanavyo
kampuni hiyo ya Kichina kuacha kufanya
shughuli kwenye eneo hilo la shule ya Magamba
na atowe taarifa kwa jeshi la polisi
Nae Meneja wa Tanroods Mkoa wa Katavi Mwandisi
Izack Kamwelwe alisema alipokea
malalamiko kutoka kwa Diwani wa kata hiyo
Philipo Kalyalya na alikwenda
kwenye eneo hilo na kuiagiza kampuni hiyo kusimamisha shughuli kwenye eneo hilo
mpaka hapo muafaka utakapo kuwa umepatikana
Alisema hata
hivyo jana Meneja wa mradi wa kampuni hiyo ya kichina alikwenda ofisini kwake
akiwa na nyaraka zinazoonyesha kampuni hiyo ilivyofuata taratibu na kupewa eneo hilo kwa ajiri ya uchimbaji wa
changalawe
Alieleza
kampuni hiyo inaonyesha kwenye mkataba huo wameisha kilipa fedha
kijiji hicho kwa ajiri ya kufanya shughuli zao hapo hata hivyo inaonyesha kuna viongozi wa kijiji hicho wamechukua
fedha kwa manufaa yao binafsi
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment