Home »
» WATAKIWA KUFUATILIA BUNGE LA KATIBA
WATAKIWA KUFUATILIA BUNGE LA KATIBA
Na Walter Mguluchuma
Katavi
Wakazi wa Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi wametakiwa kufuatilia Bunge la katiba linaloendelea iliwaweze kutambua yaliyomo kwenye Rasmu ya katiba ili wawe na uamuzi sahihi wakati wakupiga kura kwenye mikutano ya kupitisha Rasmu ya pili ya katiba
Wito huo ulitolewa hapo juzi na mwanasheria wa kituo na haki za binadamu (LHRC) Fredrick Lyimo wakati akiwahutubia wananchi wa Mji wa Mpanda kwenye viwanja vya maridadi mjini hapa
Alisema kituo hicho cha LHRC kitafanya mikutano kwenye Halmashauri zote za Mkoa wa Katavi yenye lengo la kuwahamasisha wananchi wasome rasmu ya katiba ili yale mambo ya muhimu yenye faida kwa watanzania yawekwe kwenye katiba mpya
Alifafanua kuwa endapo wananchi watafuatilia kwa kusikiliza yanayojadiliwa na wajumbe wa Bunge la Katiba linaloendelea watakuwa na uamuzi sahihi wakati utakapo fika wa kupira kura ya Rasmu ya pili ya Katiba
Lyimo alieleza yapo mambo ya msingi yenye faida na manufaa kwa watanzania ambayo yanafaa kuwekwa kwenye katiba hivyo ni vizuri wananchi wahakikishe mambo hayo yanawekwa
Alisema yapo mambo mengine ambayo wananchi watakayo yaona hayafai kwenye rasmu ya Katiba yasiyo na faida kwa Wanzania hivyo wanayo haki ya kuyakataa kwakati wa kupiga kura ya kupitisha katiba
Nae afisa habari wa LHRC Rose Mwalongo alieleza kuwa yapo mambo saba mapya ya kuungwa mkono na wananchi katika Rasmu ya Katiba
Alitataja baadhi ya mambo hayo kuwa ni kupanuliwa kwa usawa wa haki za binadamu na wananchi kuwa na mamlaka ya kupiga kura ya kkutokuwa na imani na Mnunge wao
Kwa upande wao wananchi walioshiriki kwenye mkutano huo wengi wao walisema katiba ya sasa inampa Rais madaraka makubwa hivyo ni vizuri Rais akapunguziwa madaraka hayo
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment