Home » » WASHINDA JUU YA MITI KUMKWEPA KIBOKO

WASHINDA JUU YA MITI KUMKWEPA KIBOKO

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
 
BAADHI ya wakazi wa Kitongoji cha Kashalami, Kata ya Mashimboni, Wilaya ya Mlele mkoani Katavi, wamelazimika kushinda juu ya miti kwa kuhofia kushambuliwa na Kiboko aliyevamia kijiji hicho na kutishia maisha yao.
Kwa mujibu wa Diwani wa Kata ya Mashimboni, Raphael Kalinga, tukio hilo lilitokea Agosti 18 mwaka huu, a saa 1:30 asubuhi.
Alisema kuwa mnyama huyo baada ya kuvamia kijiji hicho, alielekea kwenye nyumba ya Joseph Kashamakula ambaye alinusurika kushambuliwa wakati akitokea chooni kujisaidia.
Kwa mujibu wa Kalinga, Kiboko huyo ambaye alionekana kuwa na hasira alianza kukanyaga na vuvivunja vyombo vya mwanakijiji huyo ambavyo vilikuwa  nje ya nyumba yake na kuviharibu kabisa, jambo lililomfanya mkazi huyo apige mayowe ya kuomba msaada kwa majirani.
Hata hivyo, majirani hao walifika eneo hilo kwa ajili ya kutoa msaada, walilazimika kutimua mbio na kupanda juu ya miti baada ya kiboko huyo kuanza  kuwafuata.
Aliongeza kuwa kiboko huyo aliendelea kuzunguka eneo la kijiji hicho hadi taarifa zilipowafikia Idara ya Maliasili ya Halmashauri ya Nsimbo, ambapo walitumwa akari wa wanyama pori kwenda kumsaka wakishirikiana na wananchi na kisha kumuua kwa kumpiga risasi tumboni na kichwani.
Chanzo;Tanzania Daima 

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa