Home » » WANUSURIKA KIFO KWENYE AJARI YA BASI

WANUSURIKA KIFO KWENYE AJARI YA BASI

Na  Walter  Mguluchuma
Mpanda  Katavi
WATU kumi wamenusurika kifo baada ya gari la abiria walilokuwa wakisafiria kuacha njia na kupinduka  katika Mlima Kanono  barabara ya  Tabora – Mpanda

Kaimu Kamanda  wa Polisi Mkoa wa Katavi , Focus Malengo akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo  amebainisha kuwa majeruhi  wote  wamellazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Mpanda ,mjini Mpanda kwa matibabu .

Kwa mujibu wake  ajali hiyo ilitokea  Jumamosi , saa 11:15 jioni kilomita 40 kutoka mjini Inyonga ambao ni Makao Makuu  ya Wilaya ya Mlele katika mkoa wa Katavi ,  ambayo ilihusisha gari la abiria  liitwalo , AM Bus Service aina ya Scani mali ya Mohamed Mohamed .

Inadaiwa kuwa  gari hilo lilikuwa likitokea  mjini Tabora na kuelekea mjini Mpanda kupitia mjini Inyonga  hivyo lilipofika  katika Milima Kanono huku likiwa kasi kubwa dereva alishindwa kukata kona  na kusababisha gari hilo kumsihinda na kuacha njai na kupindika .

“Majeruhi  wote  wamelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Mpanda kwa matibabu , majina yao  bado  hayajafahamiaka kwa kuwa hali  zao  bado ni tete  ambapo miongoni  mwao  mwanamke mmoja amevunjia mkono “ aneleza Malengo

Pia anabainisha kuwa polisi  wanamsaka  dereva wa gari  hilo  ambaye jina lake bado halijafahamika ambapo alifanikiwa kutoroka katika eneo  la tukio baada ya kutokea kwa ajali  hiyo  na kujificha kusikojulikana .

“Uchunguzi wa awali umebainisha kuwa  chanzo  cha ajali  hiyo ni  uzembe upande  wa dereva  na mwendo  kasi “ anaeleza Kaimu Kamanda huyo  wa Polisi.
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa