Home »
» WANANCHI WAOMBA KATIBA MPYA IBAINISHE MAENEO YA WAFUGAJI NA WAKULIMA
WANANCHI WAOMBA KATIBA MPYA IBAINISHE MAENEO YA WAFUGAJI NA WAKULIMA
N a Walter Mguluchuma
MPANDA Katavi
Baadhi ya Wananchi wa Kata ya Kakese Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi wameomba katiba mpya ijayo kiongezwe kipengele kinacho kinachobainisha mipaka ya wafugaji na wakulima ili kuweza kumaliza migogoro ya muda mrefu ya wakulima na wafugaji
Pendekezo hilo walilitowa hapo jana mbele ya maafisa wa kituo cha sheria na haki za binadamu (LHRC)kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye kijiji cha Kakese
Mkutano huo ulioandaliwa na LHRC ulikuwa na lengo la kuwaelimisha wananchi waweze kufuatilia kwa karibu bunge la katiba linaloendelea na wasome rasmu ya katiba iliwaweze kuwa na maamuzi sahihi wakati wa kupiga kura za maoni za katiba mpya
Baadhi ya wananchi hao walisema kuwa tatizo la migogoro ya wakulima na wafugaji linasababishwa na katiba iliyopo sasa kwani haionyeshi kutenganisha maeneo ya wakulima na wafugaji
Walisema ilikumaliza migogoro ya mara kwa mara ya wakulima na wafugaji katiba mpya ijayo kiongezwe kipengele kinachobainisha mipaka ya wafugaji na wakulima
Pia walieleza wananchi wengi wamekuwa wakipoteza haki zao kutokana na kutokuwa na fedha kwa ajiri ya kuweka mwanasheria pindi wanapokuwa na kesi mahakamani hivyo kiongezwe kipengele cha kuwa kila mtu anapokuwa na kesi mahakamani serikali imweke wakili wa kumtetea kama ambavyo serikali inavyofanya kwenye kesi za mauwaji
Katiba mpya waliomba pia kiongezwe kipengele cha kuwatete na kuwalinda wazee wanaouwawa kwa kukatwa na mapanga kutokana na imani za kishirikina
Kwa upande wake mwanasheria wa kituo cha sheria na haki za binadamu LHRC Fredrick Lyimo aliwaeleza wananchi hao kuwa wanayonafasi kubwa ya kutowa maoni yao hayo kwenye Rasmu ya pili ya katiba
Nae afisa habari wa LHRC Rose Mwalongo alisema kuwa lengo la LHRC ni kuhakikisha wanawafikia wananchi na kuwapatia elimu iliwaweze kujitokeza kwa wingi kwenye kupiga kura za maoni ya Rasmu ya pili ya katiba
Alisema wananchi wanao wajibu wa kusoma Rasmu ya pili katiba iliwaweze kupata uwelewa wa kutosha na kuwafanya wapige kura ya maoni huku wakiwa na maamuzi sahihi
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment