Home »
» WATU 2086 WALIOKUWA WAKITUMIA DAWA ZA KUFUBAZA VVU WATOROKA KWENYE VITUO VYAO VYA KUPATIWA DAWA
WATU 2086 WALIOKUWA WAKITUMIA DAWA ZA KUFUBAZA VVU WATOROKA KWENYE VITUO VYAO VYA KUPATIWA DAWA
Na Walter Mguluchuma
Mpanda Katavi
Jumla ya watu 2086 Mkoani Katavi walioanzishiwa dawa za kufubaza VVU wameacha kutumia dawa hizo kutokana na sababu mbambali baada ya kuona wamekuwa na afya njema ya kunenepa miili yao
Hayo yalielezwa na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dr Yahaya Hussein hivi karibuni wakati wa afla ya kukabidhi pikipiki 24 kwa Halmashauri za Mkoa wa Katavi zilizotolewa msaada na shirika la Walter Red iliyofanyika katika viwanja vya ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi
Alisema Mkoa wa Katavi unakabiliwa na tatizo la utoro wa watu walioanzishiwa dawa za kufubaza VVU kwenye vituo vyao vya kuchukulia dawa kwa kipindi cha zaidi ya miezi mitatu pasipo kutowa taarifa yoyote kwenye vituo vyao walivyokuwa wakichulia dawa
Alifafanua Mkoa wa Katavi hadi june mwaka huu unawatoro 2086 kati ya watu 4187 ambao wanatumia dawa za kufubaza VVU
Dr Yahaya alisema athari kubwa ya utoro huo huleta usugu kwa dawa zitolewazo na hivyo kuhatarisha uwezo wa dawa zitumikazo sasa katika siku za usoni
Kwa kutambua hari hiyo jitihada mbalimbali zimewekwa za kuhakikisha kilamtumiaji wa dawa anakuwa na anwani sahihi na anakuwa na msaidizi wa kufutilia matibabu yake
Pia wamepanga kuongeza ufuatiliaji katika ngazi ya jamii ambapo mhudumu atatumia pikipiki kwenda majumbani kufahamu sababu ya mutumiaji wa dawa kwanini hakuudhuria kituoni kwake kuchukua dawa kadri alivyopangiwa tarehe ya kulipoti kituoni
Dr Yahaya alieleza Mkoa wa Katavi ni miongoni mwa Mikoa Nchini yenye kiwango cha juu cha ushamiri wa virusi vya Ukimwi ambapo kiwango cha ushamiri wa VVU katika Mkoa wa Katavi kwa sasa ni asilimia 5.9 ukilinganishwa naasilimia 5.1 ya kiwango Kitaifa
Kwa upande wake mgeni Rasmi wa afla hiyo Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dr Rajab Rutengwe alilishukuru shirika la Walter Red kwa kutowa msaada huo wa pikipiki 24 zenye thamani ya Tsh 52,800,000 kwa Halmashauri za Mkoa wa Katavi ambazo zitatumika katika kuboresha utoaji wa huduma za UKIMWI husani utoaji huduma za mikoba
DR Rutengwe alisema upatikanaji wa pikipiki hizi umekuja wakati wakati muafaka ili kuboesha huduma za za mkoba na usafirishaji wa sampuli toka kituo kimoja kwenda kingine na hatimaye ziweze fika mabara kuwafuatilia watoro wa dawa
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment