Home »
» WANAFUNZI 11 WALAZWA HOSPITALINI BAADA YA KUPATA MSHITUKO WA RISASI NA MABOMU YA POLISI KUFUATIA VURUGU ZA WAFANYABIASHARA NA POLISI
WANAFUNZI 11 WALAZWA HOSPITALINI BAADA YA KUPATA MSHITUKO WA RISASI NA MABOMU YA POLISI KUFUATIA VURUGU ZA WAFANYABIASHARA NA POLISI
Na Walter Mguluchuma
Mpanda Katavi
Wanafunzi 11 wa Shule ya Sekondari ya Mwangaza iliyopo Mjini hapa wamelazwa katika Hospital ya Wilaya ya Mpanda baada ya kupoteza fahamu kufuatia Askari wa Jeshi la Polisi kufyatua Risasi na mabomu kwenye eneo la shule hiyo baada ya kutokea vurugu katika soko la Mpanda hoteli lililojirani baina ya polisi na wafanyabiashara wa soko hilo
Tukio hilo limetokea hapo jana majira ya saa tano asubuhi katika eneo la shule hiyo lliyoko katika Mtaa wa Makanyagio mjini hapa
Chanzo cha tukio hilo ni kwamba Askari mgambo wa Halmashauri ya Mji wa Mpanda walikuwa wakifanya zoezi la kuvunjia vibada wafanyabiasha wa Soko la Mpanda Hoteli ambao wamejenga vibada sehemu zisizositahili kitendo ambacho kilipingwa na wafabiashara wa soko hilo
Wakati askari mgambo hao wakiwa wanaendelea na zoezi hilo huku wakiwa wamefuatana na Askari wawili wa jeshi la polisi walijaribu kutaka kuvuja kibanda cha mfanyabiashara mmoja ambae aliwatokea askari hao huku akiwa ameshikilia panga mbili mkononi kwa lengo la kutaka kuwashambulia askari hao huku wafanyabiashara wengine wakiwa wameshikilia mawe ambayo walianza kuwashambulia Askari hao
Baada ya muda mfupi Askari wa kutuliza gasia walifika kwenye eneo hilo la soko na kuanza kuwashambulia wafanyabiashara waliokuwa kwenye eneo hilo bila kujali kama na wao walikuwa kwenye vurugu hizo pamoja na watu waliokuwa wamefika kujipatia mahitahi hari ambayo ilifanya wafanyabiashara wakimbie na kuacha maduka n,vibanda na meza wazi
Akisimilia tukio hilo la hapo shuleni Mkuu wa Shuleni hiyo Mwalimu Simon Lubanga alisema askari hao walifika kwenye eneo la shule yake ambayo ikojirani na soko hilo na kumkuta nje mwalimu Joner joseph ambae alikuwa akiongea na simu yake ya Mkononi
Askari hao walianza kumshutumu kuwa alikuwa akitumia simu yake kwa ajiri kupiga picha za tukio hilo na alikana kufanya hivyo ndipo walipompiga kwa kitako cha bunduki na kisha kunyang’anya simu yake kitendo ambachokilimfanya mwalimu huyo kutimua mbio na kuingia darasani walimokuwemo wanafunzi wa kidato cha tatu
Alisema wanafunzi wa darasa hilo walipo una mwalimu wao amefanyiziwa kitendo hicho walitaka kuamua kutoka nje na wakati huo huo Askari wa kutuliza gasia walianza kufyatua risasi za baridi hewani katika eneo la shule
Alifafanua baada ya kufyatuliwa kwa Risasi hizo wanafunzi mbalimbali walianza kuanguka na kupoteza fahamu kutokana na mshituko wa bunduki
Mkuu wa shule alisema hari ya wanafunzi ilizidi kuwa mbaya hadi walipolazimika kuomba usafiri wa gari la wagonjwa la hospitali ya Wilaya ya Mpanda ambalo lilifika hapo lenye namba za usajiri DFP 5619 lilisaidiana na gari la Mbunge wa Mpanda mjini kuwawawisha katika hospitali ya Wilaya ya Mpanda kwa matibabu
Lubanga aliwataja wanafunzi waliolazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Mpanda kuwa ni Elizabelti Justine mwanafunzi wa kidato cha tatu ambae hari yake bado sio nzuri Milka Geoge kidato cha nne Winflida Masele kidato cha pili Maria Kasegeze kidato cha pili Anita Frenki kidato cha tatu
Wengine ni Asha Ramadhan Everada wanafunzi wa kidato cha pili Merry Bukuku , Merry Bukuku Sarafina Mwanja na Joice Martini wanafunzi wa kidato cha pili
Lubanga alisema wanafunzi hao womelazwa katika hospitali ya Wilaya ya Mpanda katika wodi namba tano na hari zao huku zikiwa zinaendelea vizuri
Alisema kutokana na hari hiyo wanafunzi wa shule hiiyo wamelazimika kusitisha masomo ya siku nzima na wamerudishwa nyumbani kwao
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment