Na Walter Mguluchuma
Mpanda Katavi
Hifadhi ya Taifa ya Katavi iliyoko katika Mkoa wa Katavi inakabiliwa na tatizo la kutembelewa na watalii wachache ukilinganisha na Hifadhi za Mikoa ya Kaskazini licha ya kujaliwa kuwa na vivutio vingi na wanyama adimu uchache huo wa watalii unachangiwa na miundombinu duni hasa barabara za ndani na nje ya Hifadhi
Hayo yalielezwa hapo juzi na Mkuu wa Idara ya Ulinzi wa Hifadhi ya Taifa ya Katavi Davis Mushi wakati akitoa taarifa ya Hifadhi hiyo kwa kipindi cha mwaka mmoja wa 2013 na 2014 wakati wa kikao cha wajumbe wa kamati ya ushauri ya Wilaya ya Mpanda kwenye ukumbi wa maji Mjini hapa
Alisema Hifadhi ya Taifa ya Katavi hupokea watalii wastani 2000 na 3,000 kwa mwaka huchache huu wa wageni huchangiwa na kuwepo kwa miundombinu duni iliyoko
Alifafanua miundombini ya utalii ndani ya hifadhi ya Katavi bado ni duni kwani sehemu za malazi ni chache ukilinganisha na mahitaji ya wageni hadi hivi sasa kuna makampuni manne tuu binafsi yanayotoa huduma ya kupiga mahema kwa wageni
Mushi alieleza kuwa kwa kipindi cha kunzia mwaka 2010 hadi mwaka 2014 hifadhi ya Katavi imetembelewa na watalii wa kutoka nje ya nchi 7,462 na watalii wa ndani 7,552 na kufanya idadi ya watalii wa ndani na nje waliotembelea hifadhi hiyo kwa kipindi cha miaka mitano kuwa ni 15,014 idadi ambayo ni ndogo ukilinganisha na Hifadhi nyingine
Alisema miundombinu hasa ya barabara ya kuja hifadhi ya Katavi ni duni kwani barabara za kutoka mikoa ya jirani ya Kigoma,Tabora na Rukwa hali inayosababisha watalii wengi kutofika Katavi ingawa kumekuwepo na jitihada za Serikali za kuboresha miundombinu kwani baadhi ya barabara zimeanza kujengwa kwa kiwango cha rami
Hifadhi hiyo imepanga mikakati mbali mbali kwa ajiri ya kuboresha utalii ili kuweza kufanya hifadhi ya Katavi iweze kutembelewa na watalii wengi zaidi
Mikakati hiyo ni kuitangaza hifadhi kupitia vyombombalimbali vya habari na kwenye maonyesho ya kimataifa na kitaifa pamoja na kwenye maonyesho ya nane nane pia kupitia bidhaa mbalimbali
Alisema Hifadhi hiyo imepanga kuanzisha utalii wa usiku ili kuwawezesha watalii kuwaona kiurasi wanyama ambao huwa hawaonekani mchana kama vile chui
Hifadhi ya Taifa ya Katavi ilianzishwa mwaka 1974 ikiwa na ukubwa kilometa za mraba 4,471 na inapatikana katika Wilaya mpya ya Mlele mkoa wa Katavi Magharibi mwa Tanzania ni hifadhi tatu kwa ukubwa Tanzania baada ya hifadhi za Ruaha na Serengeti
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment