Home »
» DC MAAFISA ELIMU KUWENI NA UTARATIBU UTARARIBU WA KUTEMBELEA SHULE
DC MAAFISA ELIMU KUWENI NA UTARATIBU UTARARIBU WA KUTEMBELEA SHULE
Na Walter Mguluchuma
Mpanda Katavi
Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Paza Mwamlima amewaagiza maafisa Elimu wa Wilaya hiyo kuwa na utaratibu wa kuzitembelea shule za Mmsingi na Sekondari ili waweze kubaina changamoto zinazozikabili shule hizo
Agizo hilo alilitowa hapo jana wakati akifungua kikao cha ushauri (DCC) cha Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda kilichofanyika kwenye ukumbi wa Idara ya maji ulioko mjini hapa
Alisema endapo maafisa Elimu watakuwa na utaratibu wa kutembelea shule zao itawasaidia kuweza kubaini changamoto zinazokuwepo kwenye shule mbalimbali
Alieleza zipo changamoto mbalimbali kwenye shule za Wilaya ya Mpanda zinazozikabili shule za msingi na Sekondari katika Wilaya huyo
Mwamlimu alisema zipo baadhi ya shule na hasa za msingi zinakabiliwa na changamoto za upungufu wa nyumba za waalimu na nyingine majengo yake yako kwenye hari mbaya na aliitolea mfano shule ya Msingi Kabungu
Alifafanua njia ya kutatua changamoto hizo ni kwa maafisa hao kutembelea kwenye shule na wakishabaini changamoto zinazokuwepo ni lazima washirikishe wananchi katika kutatua changamoto hizo
Alisema wananchi wa Wilaya ya Mpanda wako tayari kuchangia shughuli za maendeleo endapo viongozi watawashirikisha kwenye kila hatua inayokuwa imefanyika
Alieleza wananchi huwa wanakuwa wagumu kuchangia michango endapo tuu pale wanapokuwa wamechangia michango na vingozi wanaposhindwa kuwasomea mapato na matumizi ya michango yao
Hivyo viongozi wanapokusanya michango ya Wananchi wawe na utaratibu wa kuwasomea wananchi mapato na matumizi ilikutowavunja moyo wananchi za kuchangia michango mbalimbali ya shughuli za maendeleo
0 comments:
Post a Comment