Home »
» Maliasili Mpanda wakusanya zaidi ya shilingi milioni 260
Maliasili Mpanda wakusanya zaidi ya shilingi milioni 260
Na Walter Mguluchuma
Mpanda Katavi
Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda imekusanya zaidi ya shilingi milioni 260 zilizotokana na mapato ya ndani zilizokusanywa na Idara ya Ardhi na Maliasili katika kipindi mwaka mmoja kuanzia julai 2013 hadi june 2014-
Haya yalielezwa hapo juzi na Kaimu Afisa Ardhi na Maliasili na Mazingira wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda Josephina Rupia wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wa shughuli za idarahiyo kwa kipindi cha mwaka 2013 na 2014 kwenye mkutano mkuu wa mwaka wa Baraza la madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpandauliofanyika kwenye ukumbi wa maji mjini hapa
Alisema Idara hiyo imewaza kukusanya jumla ya shilingi 265,290,050 kwa kipindi cha julai 2013 hadi june mwaka huu zilizotokana na mapato ya ndani
Rupia alifafanua shilingi milioni 260,780, 000 zilitokana na ushuru wa leseni za mbao Tsh 210,750 ushuru wa Magobole ,Tsh 296,500 ushuru wa asali na kuingia polini Tsh914,000 ada ya fomu za viwanja na Tsh 3,868,800 ushuru wa uwindaji wa kienyeji
Alisema katika kipindi hicho cha mwaka mmoja idara hiyo imeweza kufanya doria mbili kubwa na kufanikiwa kukamata mbao na magongo yalivumwa bila kibali pamoja na magunia 369 ya mkaa na wanasishililia baiskeli tisa ambazo wavunaji haramu wa maliasili walikimbia na kuziacha
pia wamewaza kukamata Ng’ombe 280 ambazo zilikuwa zimeingizwa kwenye msitu wa hifadhi wa Nkaba na wamiliki watatu wa mifugo hiyo wamefunguliwa mashitaka na kufikishwa mahakamani
Josephina Rupia alilieleza baraza hilo na madiwani walikuwa wakiongozwa na mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda Yassin Kibiriti idara hiyo imeweza kufanya operesheni ya kuondoa makazi holela na watu 361 wameondolewa kwa nguvu na kati yao 15 wamefikishwa mahakamani
Alifafanua idara hiyo imefanya mpango bora wa matumizi ya adhi katika kijiji cha Lwega Tarafa ya Mwese na wanatarajia kuendelea katika vijiji vya Katuma na Kapanga
Alisema wametatua baadhi ya migogoro ya mipaka kwenye baadhi ya vijiji kwa kuzikutanisha pande zote mbili zilizokuwa na migogoro ya kugombea mipaka kwenye vijiji vyao
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:
Post a Comment