Home » » Madiwani wa muagiza mkurugenzi kuhakikisha watendaji wa Vijiji wanaitisha mikutano mikuu

Madiwani wa muagiza mkurugenzi kuhakikisha watendaji wa Vijiji wanaitisha mikutano mikuu


Na   Walter  Mguluchuma 
Mpanda  Katavi
Baraza la  Madiwani  la Halmashauri ya  Wilaya  ya  Mpanda  limemwagiza  Mkurugenzi  wa  Halmashauri  hiyo   Estomihn Changa’aha  kuhakikisha  watendaji wa vijiji  wanafanya  mikutano mikuu  kwenye  vijiji  vyao na kuwasomea wananchi  taarifa  za mapato na matumizi 

Madiwani wa Halmashauri  hiyo  walitoa  agizo hilo  hapo  jana kufutia malalamiko ya baadhi ya madiwani walioyatowa kwenye  mkutano  mkuu wa mwaka  wa  Baraza   la  Madiwani  wa kipindi  cha mwaka  2013 na 2014 ulifanyika kwenye ukumbi wa  Idara ya  Maji  mjini  hapa uliongozwa na  Mwenyekiti wa  Halmashauri hiyo  Yassin Kibiriti

Diwani  wa  Kata  ya Kabungu  Nassoro  Kasonso  ndiye  aliyekuwa wa kwanza kutowa malalamiko kwenye  baraza hilo ambapo alilamikia  kitendo cha  watendaji wa  vijiji  kutoitisha mikutano mikuu  ya Vijiji  na  mikutano ya Halmashauri kuu za vijiji kwenye maeneo  yao  kulingana na taratibu  za ratiba ya mikutano hiyo inavyoelekeza
Alisema watendaji  hao wamekuwa hawaitishi mikutano kwenye  vijiji  vyao  na  badala  yake  wamekuwa wakiandaa  mihtasari  ya uongo na  kuipeleka kwenye ofisi ya Mkurugenzi  ilikuonyesha kuwa wanafanya  mikutano kwenye vijiji vyao wakati sio kweli 

Alifafanua  watendaji hao  wamekuwa wakishirikiana  na baadhi ya wenyeviti wa vijiji  kugushi  mihtasari hiyo kwa kutumia mihtasari ya vikao vilivyopita
Nae  Diwani wa Kata ya Mpanda Ndogo  Hamad  Mapengo  alieleza  kuwa watendaji wa vijiji wamekuwa wakishindwa kuitisha mikutano mikuu kwa kuhofia  kutoa taarifa  za  mapato  na matumizi
Alisema  watendaji wengi  wa vijiji  wamekuwa ni wabadilifu  hivyo  wamekuwa  na  wasiwasi  wa  kuulizwa  maswali na  wananchi  kwenye mikutano mikuu ambao wengi wa  wananchi huwa  wanapenda  kujua hari halisi ya  mapato kwenye  vijiji vyao 

Alieleza vipo baadhi ya vijiji vinashindwa kufanya mikutano mikuu kutokana  na  vijiji  hivyo kutokuwa  na watendaji wa vijiji   na kukuta mtendaji mmoja akawa pia anakaimu  nafasi  hiyo kwenye vijiji  vingine
Kwa  upande wake  Diwani  wa  Kata ya  Karema  Michael  Kapata  alieleza  kuwa sababu  nyingine  inayochangia   watendaji wa vijiji na wenyeviti wao kuogopa kuitisha mikutano  ni kuhofia  kuhojiwa na wananchi  kuhusiana  na  tabia yao ya kuuza  adhi  za  vijiji kiholela   na hasa kwa wafugaji wa mifugo
Alisema baadhi ya viongozi  hao wamekuwa na tabia ya  kuuza  adhi  za  vijiji bila idhini  ya mikutano mikuu ya  vijiji  na  kwenye maeneo ya hifadhi za mistu hivyo wamekuwa wakihofu kuhojiwa na wananchi kwenye mikutano .

Mkurugenzi wa Halmashauri  ya Wilaya  ya Mpanda Estohn Chang’ah aliwaeleza  madiwani hao     kuwa  tayari  ameisha  anza kuwachukulia  hatua mbalimbali baadhi ya watendaji wa vijiji  ambao  wameshindwa kuwasilisha mihtasari ya mikutano  mikuu  ya vijiji  vyao
Chang’ah alitaja  baadhi ya  hatua  alizowachukulia  watendaji  hao  ni  kuwasimashia  mishahara  yao  mpaka  hapo  watakapo kuwa wamewasilisha  mihtasari kwenye  ofisi  yake na zoezi  hilo ni la kudumu katika  halmashauri yake
Aidha  Mwenyekiti wa  Halmashauri  Yassin  Kibiriti  aliwaeleza madiwani kuwa wanao wajibu  kwenye maeneo yao  kuhakikisha wanawasimia  watendaji wa vijiji  nakuhakikisha wanaitisha mikutano mikuu kwenye vijiji vilivyoko  kwenye kata zao
Alisema kama  mikutano haifanyiki  matokeo yake inakuwa ni  vigumu kwa wananchi  kufahamu na kutambua  shughuli mbalimbali  za maendeleo  zinazofanywa na  Halmashauri  hiyo
Pia  alikemea  tabia ya viongozi wa  vijiji na  vitongoji  kuacha  tabia ya kukutana pale tuu wanapojua  asilimia 20 ya fedha  za  mapato  zinapo kuwa zimepelekwa  na  Halmashauri kwenye  maeneo yao

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa