Home » » JELA MIAKA 30 KWA NYANG'ANYI WA KUTUMIA SILAHA‏

JELA MIAKA 30 KWA NYANG'ANYI WA KUTUMIA SILAHA‏

Na   Walter  Mguluchuma  
Katavi yetu blog
 Mahakama ya  Wilaya  ya Mpanda  Mkoa wa  Katavi  imemuhukumu  Emanuel Kingamkono (35) Mkazi wa Mtaa wa Nsemlwa  Mjini  Mpanda  kifungo cha miaka 30 jela  baada ya kupatikana na kosa  wizi wa kutumia silaha
Hukumu  hiyo ilitolewa hapo juzi  na Hakimu  Mkazi  wa Mahakama ya Wilaya ya Mpanda  Chiganga  Ntengwa  baada ya mahakama  kulidhika  na  ushahidi uliotolewa mahakamani hapo wa upande wa utetezi na  mashitaka
Awali  katika  kesi hiyo mwendesha  mashita   Mkaguzi wa Polisi Viriginia  Sodoka  aliiambia mahakama mshitakiwa alitenda kosa hilo  hapo  Novemba 21 mwaka jana  majira ya saa kumi jioni  katika  eneo la Kijiji  cha Kabatini
Siku  hiyo  mshitakiwa  alikuta  Esta Kasajila  eneo la Kabatini akiwa na baiskeli yake huku akiwa anatafuta mahindi mabichi kwa ajiri ya kuyanunua iliakanya biashara ya kuchoma mahindi  na kuyauza
Alieleza  mshitakiwa  alimweleza   Esta  kuwa yeye  anafahamu mahari yanapo  patikana  mahindi  hayo  na alimtaaka ampeleke  hari  ambayo ilimfanya  Esta  akubalia na  kufuatana  nae huku  akiwa na  baiskeli yake
Sodoka  alidai wakati wakiwa  wanaelekea huko  mshitakiwa alimkaba  Esta  na  kumwangusha chini na  kumpola  simu  aina ya Nokia  yenye  thamani ya Tsh 150,000  na  Baiskeli yake  hata hivyo   Esta  alifanikiwa kuponyoka na kutimua mbio huku akiwa akipiga mayowe ya kuomba msaada  huku  Emanuel akiwa anamfuguza na akiwa ameshikilia  panga ambalo alitaka kumkata   na panga hilo lilimkosa Esta na kung’ang’ania kwente mti
Esta alipata msaada kwa mtu mmoja aliyekuwa akipita kwenye eneo hilo ambae nae aliungana na Esta  kupiga mayowe na watu walifika  na kisha walikwenda kumtafuta mshitakiwa lakini hawakuweza kumkuta alikuwa ameisha tokome  huku akiwa amepola simu na baiskeli kwenye eneo hilo walikuta  panga ililo  mkosa Esta likiwa limeng’ia kwenye mti
Alieleza baada ya hapo mshitakiwa hakuonekana tena hadi hapo januari  14 mwaka huu walikutana na Esta kwenye  Soko la matunda katika mtaa wa Kawasenje  ambapo mshitakiwa  aliposemeshwa na  Esta alianza kutimua mbio hari ilipelekea wananchi wamkimbize na kufanikiwa kumkamata na kumfikisha kituo cha polisi cha Mpanda ambako  toka awali tukio hilo lilikuwa limeisha funguliwa
Mshitakiwa katika utetezi wake aliomba  mahakama imwachie huru kwani yeye hakutenda  kosa hilo   na amesingiziwa  tuu kwa kufananishw
Hakimu  Chiganga  Ntengwa baada ya  utetezi huo alisoma hukumu kwa kuimbia mahakama  kuwa   kutokana na ushahidi uliotolewa  mahakamani   mshitakiwa  amepatikana  ya kifungu  cha sheria  287 A  cha kanuni ya  adhabu    sura ya 16 ya marekebisho ya mwaka  2009 hivyo mahakama imemuhumu  Emanueli Kingamkono kwenda jela kifungo cha miaka 30 jela


Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa