Home » » HATARI: MTU MZIMA WA MIAKA 52 AJINYONGA KWA MTANDIO BAADA YA KUACHWA NA MKEWE

HATARI: MTU MZIMA WA MIAKA 52 AJINYONGA KWA MTANDIO BAADA YA KUACHWA NA MKEWE



Na  Walter   Mguluchuma
Katavi yetu Blog
Mtu mmoja  aliyefahamika kwa jina  la  Joseph  Lukato (52) Mkazi wa kijiji  cha  Vikonge  Kata ya Mpanda Ndogo Wilaya ya Mpanda  amekutwa  akiwa amejinyonga   kwenye mti kwa kutumia  kipande cha mtandio wa kitambaa cha nguo baada ya kupata hasira ya kuachwa na mkewe
Kwa mujibu wa Kaimu Kamanda wa jeshi la polisi Mkoa wa Katavi Focas Malengo tukio hilo lilitokea hapo  julai  27 mwaka huu majira ya saa mbili asubuhi kijijini hapo  katika shamba la jirani yake na marehemu
undani wa tukio  wa tukio hili ni kwamba   marehemu alikuwa na ugomvi wa muda mrefu na mkewe aitwaye   Mary  Joseph (42)aliyekuwa akimtuhumu kuwa na mausiano  ya kimapenzi na mwanaume mwingine kijijini hapo
Alisema  julai  19 marehemu  alirudi  nyumbani kwake  akitokea shambani  majira ya saa nane mchana  na kula chakula ambacho anadai mkewe alipika chakula hicho hakikuwa kimeiva
Ndipo ulipoanza ugomvi wa wanandoa hao  wawili  ambapo marehemu alimtuhumu  mkewe  kuwa amempikia  chakula kibicha kwa kuwa alichelewa kurudi  nyumbani  kwa kuwa alikuwa kwa  mwanaume mwingine mwenye mahusiano nae ya kimapenzi
Malengo alialeza  mkewe alijitahidi kujijitetea kuwa hakuwa ametoka siku hiyo nyumbani kwake na wala chakula alichompia sio kibichi bali kimeiva
Alisema hata hivyo marehemu  hakukubaliana na mkewe  hivyo aliendelea kumshutumu tuu mkewe na kisha alimpa kichapo
Ugomvi wa wanandoo hao uliendelea kwa muda mrefu siku hiyo   na ndipo mke wa marehemu alipoamua kurudi nyumbani kwa wazazi wake  kwa kuhofia usalama wa maisha yake
Marehemu alijitahidi kufanya jitihada za mara kwa mara  za kumshawishi mkewe arudi nyumbani kwake ili wakaendelee kuishi kama walivyokuwa wakiishi maishayao ya mume  na mke hata hivyo  Mary alimkatalia katakata kurudi kwa  marehemu
 Alisema mke wa  marehemu alipokuwa nyumbani kwao aliendelea na shughuli zake kama kawaida hadi hapo julai 27  alipewa taarifa  za kifo cha mume wake  kupitia  kwa  jirani yake na marehemu aitwaye  Anton  Katwana
Kaimu Kamanda  Malengo alieleza mwili wa marehemu  umefanyiwa uchunguzi wa kidakitari na tayari wamekabidhiwa ndugu wa marehemu kwa ajiri ya taratibu za mazishi

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa