Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
MKUU wa Wilaya (DC) ya Mpanda, Paza Mwamlima, amewataka vijana
kujiunga na mafunzo ya VETA wanapomaliza elimu ya msingi, ili
waweze kupata elimu ya kujiajiri.
Mwamlima alitoa wito huo juzi kwenye Kijiji cha Kasekese, wilayani
hapa wakati akifungua kambi ya vijana waliojitolea kufyatua matofali,
kusomba mawe na mchanga kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa
10 ya Shule ya Msingi ya Kasekese na bweni la sekondari ya Mpanda
Ndogo.
Alisema vijana wana wajibu wa kutambua kuwa taifa linawategemea,
hivyo wanapaswa kujishughulisha katika kazi mbalimbali za ujenzi wa
taifa.
Alisema mataifa yote duniani yanajengwa na yalijengwa na vijana,
hivyo wana wajibu wa kuutumia vizuri ujana wao kuliendeleza taifa.
Alisema vijana wa Mpanda wana nafasi kubwa ya kuanzisha shughuli za kiuchumi kutokana na fursa zilizopo.
Hata hivyo, alisema vijana wengi hawana ardhi, hivyo vijiji
vyote vinatakiwa kuwapatia ardhi vijana, na kwamba zoezi hilo
lifanyike kwa ushirikiano baina ya Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda na
vijiji husika.
Chanzo:Tanznia Daima
0 comments:
Post a Comment