Home » » Wagombea kuzika mwili wa Marehemu mtoto mwenye umri wa mwaka mmoja na nusu

Wagombea kuzika mwili wa Marehemu mtoto mwenye umri wa mwaka mmoja na nusu

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Na Walter Mguluchuma
Mpanda Katavi
Mtafaruku mkubwa umetoke msibani katika Mtaa wa Kawajense madukani Wilayani Mpanda Mkoa wa Katavi baada ya ndugu wa pande mbili kugombania  kuzika mwili wa mtoto aitwaye  Junia Bacho  mwenye umri wa mwaka mmoja  na nusu aliyefariki june 26majira ya saa saba usiku  katika Hospitali ya Wilaya ya Mpanda
Tukio hilo la ambalo   lilivutia hisia za watu wengi  lilitokea hapo juzi  katika mtaa huo baada ya marehemu huyo   kufariki akiwa amelazwa katika hospitali ya Wilaya ya Mpanda aliko kuwa akiuguzwa na shangazi yake aitwaye  Evelyne Komba
Baada ya mtoto huyo kufariki  kulitokea  kutoelewa baina ya ndugu wa baba wa mtoto  aitwaye  Joseph Bacho na ndugu wa  mama wa marehemu aitwaye  Anna Kizo
Upande  wa ndugu wa baba ulidai  wao ndio wenye haki ya   na jukumu la kuchukua mwili wa marehemu na kuupeleka  nyumbani kwa mama mzazi wa baba wa marehemu aitwaye  Ted Francis(bibi miti)  anae ishi katika mtaa wa madukani mjini hapa
Ndugu wa mama wa marehemu nao walidai  hawako tayari msiba huo kwenda kwa baba wa marehemu  kwani hakuwa na uhalali wa  chukuchua mwili wa marehemu kwa kile walicho dai baba wa marehemu alikuwa ajatowa mahari hivyo wao awamtambui
Hari hiyo iliwafanya ndugu wa pande hizo mbili  kuanza kutupiana shutuma za lawama  ambapo ndugu wa baba wa marehemu  walimshutumu mama wa marehemu kwa kushindwa kumuudumia  marehemu wakati akiwa  mgonjwa na muda wote baba wa marehemu  alipokuwa akifika nyumbani  Anna  Kiza  alikuwa hamrusu kumwona mwanae kwa kumweleza amelala
Walidai toka marehemu alipochukuliwa na baba yake  hapo june 18 kwa ajili ya kumshughulikia  matibabu ya ugonjwa  wa ukosefu wa lishe(kashakoo) mama wa  marehemu wala ndugu wa upande  wake  hawakuwahi kufika hata siku moja kumwangalia hari iliyofanya mtoto huyo awe  anaangaliwa na shangazi  Evelyne  yake na bibi yake  Ted
Pamoja  na maelezo hayo  ndugu wa mama wa marehemu waliendelea na msimamo wao wa msiba  kuwa kwao  baada ya mabishano ya muda mrefu pande mbili hizo ziliamua kuuwacha mwili wa marehemu kwenye chumba cha kufidhi maiti katika hospitali ya Wilaya ya Mpanda
Baaada ya kurudi  nyumbani kila upande uliweka  msiba  nymbani kwao hali iliyofanya msiba huu kuwekwa sehemu mbili tofauti katika mtaa mmoja
Siku iliyofuata wazee wa mtaa huo waliingilia kati  mgogoro na  kufanya kikao na pande mbili hizo zilizokuwa zikivutana  na kufikia uamuzi wa  kuwa msiba huo uwe nyumbani kwao na baba wa marehemu
Kufutia uamuzi huo shangazi wa marehemu  Evelyne Komba aliongoza ndugu  na kwenda  chumba cha kuhifadhi maiti na kuuchukua mwili wa marehemu na kuupeleka kwao na baba wa marehemu kwa ajiri ya maandalizi ya mazishi yaliyokuwa yamepangwa kufanyika juzi saa nane  kwenye makaburi ya kawanjense msufini
Wakati huo shughuli za uchimbaji wa kaburi ulifanyika na kaburi lilikamilika  ikawa unasubiliwa muda uliopangwa wa kufanyika kwa mazishi
Baada ya muda mfupi ndugu  wa baba wa marehemu  walipata taarifa kuwa kaburi walilochimba kwa ajiri ya kumzikia marehemu wameonekana watu wakilifukia  hari ambayo iliwafanya waelekee huko makaburini
Ndugu hao wa baba wa marehemu walipofika makaburini walikuta dada wa mtoto wa marehemu  aaitwaye  Jane Kiza na wenzaki wakiwa ndio wanamalizia kufukia kaburi hilo ambalo halikuwa na mwili wa marehemu
Jane na kundi lake walipoulizwa kwanini wamefukia kaburi hilo  walianza kufoka  na kisha kundi la ndugu wa mama wa marehemu  walitokea hapo na kuanza kuwashambulia kwa kipigo ndugu wa baba wa marehemu
Askari wa kikosi cha kutuliza ghasia walikuwa wameongozwa  na meja wao  alijulikana kwa jina la Bahati   walifika kwenye eneo hilo na kutuliza ghasia  hizo  na kisha walielekea eneo la msibani na kuamuru mwili huo wa marehemu urudishwe kwenye  chumba cha kuifadhi maiti hadi hapo ufumbuzi wa tatizo hilo utakapo kuwa umekwisha
Ndugu wa marehemu walikubaliana  na uamuzi huo wa kuurudisha mwili wa marehemu kwenye cgumba cha kuifadhi maiti

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa