Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Na Walter
Mguluchuma
Mpanda Katavi
Mtafaruku mkubwa
umetoke msibani katika Mtaa wa Kawajense madukani Wilayani Mpanda Mkoa wa
Katavi baada ya ndugu wa pande mbili kugombania
kuzika mwili wa mtoto aitwaye
Junia Bacho mwenye umri wa mwaka
mmoja na nusu aliyefariki june 26majira
ya saa saba usiku katika Hospitali ya
Wilaya ya Mpanda
Tukio hilo la
ambalo lilivutia hisia za watu
wengi lilitokea hapo juzi katika mtaa huo baada ya marehemu huyo kufariki akiwa amelazwa katika hospitali ya
Wilaya ya Mpanda aliko kuwa akiuguzwa na shangazi yake aitwaye Evelyne Komba
Baada ya mtoto
huyo kufariki kulitokea kutoelewa baina ya ndugu wa baba wa
mtoto aitwaye Joseph Bacho na ndugu wa mama wa marehemu aitwaye Anna Kizo
Upande wa ndugu wa baba ulidai wao ndio wenye haki ya na jukumu la kuchukua mwili wa marehemu na
kuupeleka nyumbani kwa mama mzazi wa baba
wa marehemu aitwaye Ted Francis(bibi
miti) anae ishi katika mtaa wa madukani
mjini hapa
Ndugu wa mama wa
marehemu nao walidai hawako tayari msiba
huo kwenda kwa baba wa marehemu kwani
hakuwa na uhalali wa chukuchua mwili wa
marehemu kwa kile walicho dai baba wa marehemu alikuwa ajatowa mahari hivyo wao
awamtambui
Hari hiyo
iliwafanya ndugu wa pande hizo mbili
kuanza kutupiana shutuma za lawama
ambapo ndugu wa baba wa marehemu
walimshutumu mama wa marehemu kwa kushindwa kumuudumia marehemu wakati akiwa mgonjwa na muda wote baba wa marehemu alipokuwa akifika nyumbani Anna Kiza alikuwa
hamrusu kumwona mwanae kwa kumweleza amelala
Walidai toka
marehemu alipochukuliwa na baba yake
hapo june 18 kwa ajili ya kumshughulikia
matibabu ya ugonjwa wa ukosefu wa
lishe(kashakoo) mama wa marehemu wala
ndugu wa upande wake hawakuwahi kufika hata siku moja kumwangalia
hari iliyofanya mtoto huyo awe
anaangaliwa na shangazi Evelyne yake na bibi yake Ted
Pamoja na maelezo hayo ndugu wa mama wa marehemu waliendelea na
msimamo wao wa msiba kuwa kwao baada ya mabishano ya muda mrefu pande mbili
hizo ziliamua kuuwacha mwili wa marehemu kwenye chumba cha kufidhi maiti katika
hospitali ya Wilaya ya Mpanda
Baaada ya
kurudi nyumbani kila upande uliweka msiba
nymbani kwao hali iliyofanya msiba huu kuwekwa sehemu mbili tofauti
katika mtaa mmoja
Siku iliyofuata
wazee wa mtaa huo waliingilia kati
mgogoro na kufanya kikao na pande
mbili hizo zilizokuwa zikivutana na
kufikia uamuzi wa kuwa msiba huo uwe
nyumbani kwao na baba wa marehemu
Kufutia uamuzi
huo shangazi wa marehemu Evelyne Komba
aliongoza ndugu na kwenda chumba cha kuhifadhi maiti na kuuchukua mwili
wa marehemu na kuupeleka kwao na baba wa marehemu kwa ajiri ya maandalizi ya
mazishi yaliyokuwa yamepangwa kufanyika juzi saa nane kwenye makaburi ya kawanjense msufini
Wakati huo
shughuli za uchimbaji wa kaburi ulifanyika na kaburi lilikamilika ikawa unasubiliwa muda uliopangwa wa
kufanyika kwa mazishi
Baada ya muda
mfupi ndugu wa baba wa marehemu walipata taarifa kuwa kaburi walilochimba kwa
ajiri ya kumzikia marehemu wameonekana watu wakilifukia hari ambayo iliwafanya waelekee huko
makaburini
Ndugu hao wa baba
wa marehemu walipofika makaburini walikuta dada wa mtoto wa marehemu aaitwaye
Jane Kiza na wenzaki wakiwa ndio wanamalizia kufukia kaburi hilo ambalo
halikuwa na mwili wa marehemu
Jane na kundi
lake walipoulizwa kwanini wamefukia kaburi hilo
walianza kufoka na kisha kundi la
ndugu wa mama wa marehemu walitokea hapo
na kuanza kuwashambulia kwa kipigo ndugu wa baba wa marehemu
Askari wa kikosi
cha kutuliza ghasia walikuwa wameongozwa
na meja wao alijulikana kwa jina
la Bahati walifika kwenye eneo hilo na kutuliza
ghasia hizo na kisha walielekea eneo la msibani na
kuamuru mwili huo wa marehemu urudishwe kwenye
chumba cha kuifadhi maiti hadi hapo ufumbuzi wa tatizo hilo utakapo kuwa
umekwisha
Ndugu wa marehemu
walikubaliana na uamuzi huo wa
kuurudisha mwili wa marehemu kwenye cgumba cha kuifadhi maiti

No comments:
Post a Comment