Monday, June 30, 2014

DC:VIJANA JIUNGENI NA VETA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

MKUU wa  Wilaya (DC) ya Mpanda, Paza  Mwamlima, amewataka  vijana  kujiunga  na mafunzo  ya  VETA wanapomaliza elimu ya msingi, ili  waweze kupata elimu ya kujiajiri.
Mwamlima alitoa wito huo juzi kwenye Kijiji cha Kasekese, wilayani  hapa   wakati akifungua kambi ya vijana waliojitolea kufyatua matofali, kusomba  mawe na mchanga  kwa ajili ya ujenzi wa  vyumba vya madarasa 10 ya Shule ya Msingi ya Kasekese  na bweni la sekondari ya Mpanda Ndogo.
Alisema vijana wana wajibu wa kutambua kuwa taifa linawategemea, hivyo wanapaswa kujishughulisha katika kazi mbalimbali za ujenzi wa taifa.
Alisema mataifa yote duniani  yanajengwa  na yalijengwa  na vijana,  hivyo  wana wajibu wa kuutumia vizuri ujana wao kuliendeleza taifa.
Alisema vijana wa Mpanda wana nafasi kubwa ya kuanzisha  shughuli  za kiuchumi  kutokana na fursa zilizopo.
Hata hivyo, alisema vijana wengi hawana ardhi,  hivyo  vijiji  vyote  vinatakiwa kuwapatia  ardhi vijana, na kwamba zoezi hilo  lifanyike kwa ushirikiano baina ya Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda na vijiji husika.
Chanzo:Tanznia Daima 

No comments:

Post a Comment