Saturday, June 28, 2014

TUME YA UCHAGUZI KUONGEZA VITUO VYA KUJIANDIKISHIA WAPIGA KURA‏

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Na Walter Mguluchuma
Mpanda Katavi
Tume ya uchaguzi  imeongeza  vituo vya  kuandikisha  vya kupigia  kura  katika  uboreshaji wa daftari  la wapiga kura  kutoka vituo  24,919 hadi kufikia vituo  40,015
Haya yalisemwa hapo juzi na Kamishina wa Tume ya Taifa ya uchaguzi  Prof  Amon  Chaligha  wakati  akifungua kikao cha   tume ya Taifa ya uchaguzi na waandishi wa habari wa  Mkoa wa Katavi kilichofanyika  kwenye ukumbi wa Idara ya Maji mjini hapa
Alisema  tume ya uchaguzi  inatarajia  kufanya uboreshaji  wa Daftari la  kudumu  la wapiga  kwa awamu ya kwanza hivi karibuni  kwa kutumia  Teknolojia  mpya  ya  Blometric voter  Registration(BVR)kwa ajiri ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2015
Alifafanua  uandikishaji wa  sasa utafanyika  katika  vituo  vilivyo katika ngazi  ya Vitongoji  Vijijin na mitaa tofauti na ilivyo kuwa  huko nyuma
Prof Chaligha  alieleza  uandikishaji wa  huko awali ulikuwa ukifanyika kwenye  ngazi ya Kata  hivyo kwa utaratibu wa sasa  vituo  vya kujiandikishia  vimeongezeka  kutoka 24,919 na kufikia  40,015
Lengo la kuongeza  vituo   ni  kuwawezesha watu  kuwa  karibu  zaidi  na vituo vya kujiandikishia  na hivyo itapunguza  malalamiko  ya wananchi  ya kulalamikia kuwa vituo viko mbali na wanako ishi
Alisema Tume ya uchaguzi kwa kuongeza vituo  na kuvisogeza karibu na wannchi  wanayomatumaini  wajiandikishaji  wataongezeka  na mwamko  wa kupiga kura utakuwa ni mkubwa

No comments:

Post a Comment