Home » » WATATU WASHIKILIWA NA POLISI KWA TUHUMA ZA KUCHINJA BODADODA NA KUMPOLA PIKIPIKI

WATATU WASHIKILIWA NA POLISI KWA TUHUMA ZA KUCHINJA BODADODA NA KUMPOLA PIKIPIKI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Na  Walter  Mguluchuma
Mpanda Katavi
Jeshi  la Polisi Wilayani Mpanda Mkoa wa Katavi  linawashikilia watu watatu kwa tuhuma za kumuuwa Bodaboda  mmoja aitwaye Frenk  Joseph (25)mkazi wa mtaa wa Nsemlwa Wilayani Mpanda Mkoa wa Katavi  kwa kumchinjashigo  na kisha kumpola pikipiki  yake  aina ya  SANLG  yenye namba za  usajiri  T 704 CDQ
Kamanda wa jeshi la Polisi wa Mkoa wa KataviKamishina msaidizi  mwandamizi  Dhahiri Kidavashari aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni  Charles  Kidaha(29),Madia Mtema (40) na Buyenza  Jendesha (40) wote wakazi wa Tarafa ya Mwese Wilayani Mpanda
Kidavashari  alisema  watuhumiwa hao  walimuuwa bodaboda huyo  hapo  Aprili  26 mwaka huu majira ya saa saa kumi na moja jioni huko katika eneo la Kijiji cha Mpembe Tarafa ya Mwese  Wilayani Mpanda
Siku hiyo ya tukio  marehemu Samwel  alikuwa kwenye  kijiwe chake cha Bodaboda kilichoko kwenye hospitali ya Wilaya ya Mpanda akiwa na pikipiki yake aina ya  Sunlg  yenye  Namba za usajiri  T704CDQ a
  Alisema wakati  akiwa kwenye kituo hicho   cha Bodaboda  alitokea mtu asiye fahamika na kumkodisha marehemu  ambapo waliondoka nae   huku marehemu akiwa aja waagabodaboda  na kuwafahamisha mahari alikokuwa  wakielekea  na mteja wake huyo
Alifafanua kuwa ndipo siku iliyofuata ya tarehe 27 Aprili  mwili wa marehemu bodaboda huyo  ulipoonekana  ukiwa umetelekezwa  porini  katika kijiji  cha Mpembe  huku  akiwa amechinjwa na kitu chenye ncha kali  na pikipiki yake haikuonekana  katika  eneo hilo
Kamanda Kidavashari  alieleza  kuwa baada ya  tukio la mauwaji hayo  polisi waliendelea kufutilia tukio hilo kwa kushirikiana na  raia wema  na ndipo hapo  mei 22 majira ya  saa kumi na moja jioni  huko katika kijiji  cha Kasekese  Kata ya Simbwesa  Wilaya ya Mpanda  raia wema walitowa taarifa kwa jeshi la polisi  kuwa wanamashaka  na watuhumiwa hao kwani waliwasili kijijni hapo wakiwa wamepakizana kwenye pikipiki moja
Alisema baada ya taarifa hizo jeshi la polisi liliweza kufanikiwa kufika kijijini  hapo mara tuu baada ya muda mfupi  na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa  wote watatu wakiwa na pikipiki hiyo ya marehemu  Samweli waliompola baada ya kumuuwa
Katika maojiano ya awali baini ya jeshi la polisi  na watuhumiwa hao watatu  imeonyesha  kuwa  watuhumiwa hao  ndio waliohusika   na mauwaji ya bodaboda huyo
Kamanda Kidavashari ameleza  watuhumiwa  hao  wote watatu  wanatarajiwa  kufikishwa mahakamani  baada ya  upelelezi  kukamiliki

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa