Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
POLIISI wilayani Mpanda, Katavi linawashikilia watu watatu kwa
tuhuma za kumuua dereva wa pikipiki ‘Bodabodai, Frank Joseph (25), mkazi
wa mtaa wa Nsemlwa kwa kumchinja shigo na kisha kumpora pikipiki yake.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi, Kamishina Msaidizi Mwandamizi,
Dhahiri Kidavashari, aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Charles
Kidaha(29), Madia Mtema (40) na Buyenza Jendesha (40) wote wakazi wa
Tarafa ya Mwese, wilayani Mpanda.
Kidavashari alisema watuhumiwa hao walimuuwa dereva wa pikipiki T 704
CDQ Sanlg, Aprili 26 mwaka huu, saa 11 jioni, eneo la Kijiji cha
Mpembe.
Alisema siku ya tukio dereva huyo wa pikipiki alikuwa kwenye kijiwe
chake cha kilichopo hospitali ya Wilaya ya Mpanda na alitokea mtu
asiyefahamika na kumkodisha na hakuonekana hadi siku iliyofuata akiwa
amemuawa na maiti yake kutelekezwa porini katika kijiji cha Mpembe.
Alisema polisi kwa kushirikiana na raia wema Mei 22 walipata taarifa
kuwepo kwa watuhumiwa hao, kwani waliwasili kijijni hapo wakiwa
wamepakizana kwenye pikipiki hiyo. Watuhumiwa hao wanatarajiwa
kufikishwa mahakamani baada ya upelelezi kukamilika
Chanzo;Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment