Home » » WATATU WAFARIKI HAPO HAPO KATIKA AJALI YA FUSO.

WATATU WAFARIKI HAPO HAPO KATIKA AJALI YA FUSO.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

N a  Walter  Mguluchuma-Katavi yetu Blog
Mpanda Katavi
 Watu  watatu wamefariki  dunia  hapo hapo Wilaya Mpanda Mkoa wa Katavi   baada ya gariRoli aina ya Fuso   walilokuwa wakisafiria kupinduka  na watu wengine wanne wamejeruhiwa  na kulazwa  katika  Hospitali ya Wilaya ya Mpanda
Ajari hiyo ilitokea hapo  juzi  majira ya saa  kumi na moja jioni  baada ya gari  aina ya fuso  lenye  Nanba za usajiri T 168 APU  lililokuwa likiendeshwa na Dreva   Deus Lukas  (28 )mkazi wa mtaa wa Kawajense Mjini hapa kupinduka  katika  mlima wa Sijonga  Gari  mali ya mtu mmoja mkazi wa kijiji cha Ikola alifahamika kwa jina moja tuu (MAN) 
Katika hajari hiyo  watu watatu  walikufa hapo hapo  ambao Kamanda wa polisi  wa Mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashari aliwataja  kuwai  ni Agnes Martin(7) mwanafunzi wa shule ya Msingi Kashato  katika Halmashauri ya mji wa Mpanda Elizabeti Mseveni (24) mkazi wa Mtaa wa Majengo  mjini Mpanda ambae ni mama mdogo wa  Agnes   na Madanganya Rashid (53) mkazi wa kijiji  cha Ikola  Tarafa ya Karema Wlaya ya Mpanda
Kamanda wa Jeshi  la Polisi wa Mkoa wa Katavi  Dhahiri Kidavashari  alisema  ajari hiyo  ilitokea  katika eneo la Mlima wa Sijonga  Katika  Tarafa ya Kabungu Barabara  inayotoka mjini  Mpanda Kuelekea  Tarafa ya Karema mwambao mwa Ziwa Tanganyika baada ya gari hilo kukatika propelashafuti  likiwa  likiwa kwenye mlima
Kidavashari aliwataja watu  wanne waliojeruhiwa ambao wamelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Mpanda  kuwa ni  Saimoni  Masafila (42)Mkazi wa  Kijiji cha Mwamapuli Tarafa ya Mpimbwe Wilaya ya Mlele  Mwasiti   Juma  (19) Mwajuma Seif  (19) na Nassir Salumu  mtoto  mdogo wa miezi minne wote wakazi wa mjini  Mpanda
Alisema Dreva wa gari hilo  Deus Lukas  alikuwa akiendesha Fuso  hilo  huku akiwa amewapakia watu hao na mizigo mbalimbali ya bidhaa za wafanyabiashara huku akiwa anatokea mjini Mpanda akiwa anaelekea katika kijiji  cha Ikola kilichoko mwambao mwa ziwa Tanganyika
Kidavashari  alifafanua  baada ya gari hilo kufika kwenye eneo la mlima wa Sijonga  gari hilo lilikatika fropela shafuti  na kusababisha roli hilo kupinduka  na  watu watatu walifariki Dunia hapo hapo na watu  wanne walijeruhiwa   na kulazwa katika hospitali ya Wilaya ya Mpanda wakiendelea  kupatiwa matibabu huku hari zao zikiwa zinaendelea vizuri
Alisema  Dreva wa  Gari hilo  alikamatwa  na anaendelea  kushikiliwa na jeshi la polisi wakati taratibu za kumfikisha mahakamani zikiwa zinaendelea  ili akajibu mashitaka ya kuhusiana na ajari hiyo
Kidavashari alieleza  mili ya marehemu  wote watatu  imehifadhiwa katika  chumba  cha  kuhifadhi maiti  katika Hospitali ya Wilaya yaMpanda kwa ajiri ya kufanyiwa uchunguzi wa Kidaktari na baada ya hapo watakabidhiwa ndugu kwa ajiri ya mazishi

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa