Home » » Mkuu wa mkoa azindua mchakato wa uanzishwaji wa mfuko wa jamii kwa tiba ya kadi TIKA

Mkuu wa mkoa azindua mchakato wa uanzishwaji wa mfuko wa jamii kwa tiba ya kadi TIKA

Baadhi ya washiriki wa mkutano wa kongamano la uzinduzi rasmi wa mchakato wa uanzishwaji wa mfuko wa afya ya jamii tiba kwa kadi (TIKA) wakiwa kwenye mkutano uliofanyika jan kwenye Ukumbi wa Idara ya maji wakimsikiliza kwa makini mkuu wa mkoa wa katavi Dr. Rajabu Lutengwe ambaye hayupo pichani wakati akitoa hotuba ya uzinduzi rasmi wa mchakato wa uanzoshwaji wa mfuko wa jamii tiba kwa kadi.

Katibu wa chama cha walemavu Godfrey Sadala akichangia mawazo kwenye kikao cha wadau wa uzinduzi rasmi wa mchakato wa uanzishaji wa bima ya afya ya jamii  tiba kwa kadi(TIKA) uliozinduliwa jana katika ukumbi wa Idara ya maji mjini mpanda na kuwashirikisha wadau mbalimbali, ambapo aliulizia namna ya walemavu watakavyonufaika na mfuko huo. Uzinduzi huo rasmi uliwashirkisha wadau mbalimbali wa mji wa mpanda na kupokewa kwa furaha na washiriki wa kongamano hilo ambapo mgeni rasmi alikuwa mkuu wa mkoa wa Katavi Dr. Rajabu Lutengwe.
Picha na Walter Mguluchuma


Na  Walter   Mguluchuma
Mpanda  Katavi
Mkuu wa Mkoa wa    Katavi  DR  Rajabu Rutengwe  amezindua  Rasmi mchakato  wa uanzishwaji  wa Mfuko wa   Afya  ya Jamii ya Tiba  kwa njia ya   kadi  TIKA   katika Halmashauri ya  Mji wa Mpanda Mkoa wa Katavi   
Uzinduzi  huo ulifanyika  hapo jana  katika ukumbi wa  Idara ya  maji   ambapo ndio ilikuwa ni siku ya wadau  wa   Mji wa Mpanda 
Mkuu  wa Mkoa   Dr  Rutengwe  katika   hotuba  yake ya  ufunguzi  kwa   wadau  wa mchakato  wa uanzishwaji  wa sheria ndogo  na hati rasmi ya  mfuko  wa Afya  ya Jamii  kwa kadi kwa  mji  Mpanda  aliwataka  wadau  watambue umuhimu  wa mpango  wa uchangiaji  kabla ya kuugua
Alisema  ni  vizuri  wadau wakaharakisha   kupitisha  mchakato huo  wa kutunga  sheria  ndogo  ili  ianze  kutumika  kwa wananchi  wa Mji wa  Mpanda  na waweze kunufaika  na  mfuko huo  kama  ambavyo wanavyo  nufaika watu wa  Miji mingine wanao tumia  mfuko huo
Alieleza  mpango kwa  Tiba  kwa kadi  utakuwa na manufaa kwa wakazi wa Mji wa   Mpanda  kwani  mpango huo ni  mzuri  na hasa  kwa watu wenye  kipato kidogo  kwa kuchangia  kiasi cha  shilingi   elfu kumi  kwa mtu  mmoja  kwa mwaka mzima  na  kiasi hicho  kinamfanya  mchangiaji apate  matibabu  kwa kipindi cha mwaka  mzima
Aidha  aliutaka  Mfuko  wa    Bima  ya    Afya  NHIF iandae  utaratibu  mzuri wa  kuweka  kumbukumbu  za wanachama  wa TIKA   na  wawe  na mpango endelevu  wa kutoa elimu  mara  kwa mara  kwa makundi mbalimbali  ili kuwahamasisha wajiunge na   mfuko wa TIKA
Pia  aliiangiza  Halmashauri ya  mji wa Mpanda  kuhakikisha  asilimia  67 ya  fedha   zinazo patikana  zinanunuliwa ndawa kwani haitakuwa vema  fedha hizo wakazitumia kwa wanufaa  mwngine   na kusababisha  wanachama kukosa dawa  pindi waunguapo na  matokeo yake wanaweza  wakasababisha  watu wakauchukia mfuko huo  pasipo na sababu
Alisema  iandae utaratibu  wa kuzijua  familia  ambazo  zina hari  hari ngumu  kiuchumi  ambazo  zinashindwa  kuchangia  katika mpango huu  na wakisha  zitambua  Halmashauri  iweke  utaratibu wa kuzichangia  familia hizo  kwani hari ya upatikanaji wa dawa  katika  hospitali  na kwenye vituo vya Afya  na  zahati  katika Mkoa wa Katavi sio  wakuridhisha
Kwa  upande wake  mwakilishi wa  wa   kaimu Mkurugenzi wa  wa  Mfuko wa    Bima  ya Afya  NHIF   Celestini  Muganga  alieleza  kuwa jumla ya Halmashauri   128  zilizopo hapa  nchini  zinanufaika  na  mfuko huo  kati ya Halmashauri   168   zilizopo hapa  nchini
Alisema   lengo la  mfuko  huo ni kuhakikisha    wanachama wake hawakosi dawa pindi wanapo kuwa wameugua   na ndio maana  mfuko huo umeweka  utaratibu wa kuzikopesha fedha   Halmashauri  kwa  ajiri ya kununulia  dawa   na pia wanatowa zaidi kwa Halmashauri ambayo  iliyoongoza kwa kuingiza wanachama wappya
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Paza   Mwamlima   alisema ipotabia kwa baadhi ya    watumishi wa  idara ya Afya  kuwanyanyasa  watu wanakwenda  kutibiwa  kwenye hospitali    vituo  vya   afa  na Zahanati   kwa kutumia  kadi 

Wil aya ya  Mpanda   ni miongoni mwa Halmashauri   40  hapa  nchini  ambazo  zilikuwa   hazijajiunga  na   mfuko wa  wa  Af ya  ya Bima ya   jamii TIKA  na  hari ambayo ilisababisha wakazi wa mji huu kukosa huduma hii  muhimu
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa