Home » » MAKAO MAKUU YA HALMASHAURI YA WILAYA YA MPANDA KUHAMIA KABUNGU‏

MAKAO MAKUU YA HALMASHAURI YA WILAYA YA MPANDA KUHAMIA KABUNGU‏

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Na   Walter Mguluchuma 
Mpanda  Katavi
Baraza la  Madiwani la Halmashauri ya  Wilaya  ya Mpanda  Mkoa wa Katavi  limepitisha uamuzi  wa  kuhamisha Ofisi  za Makao yake   makuu   ya Halmashauri hiyo  kutoka   Mjini    Mpanda  na  kuhamishia   makao makuu  yake   mapya   katika    Tarafa  ya Kabungu  Wilayani
Uamuzi huo ulitolewa   hivi  karibuni   katika   kikao  cha  Baraza la  Madiwani  la  Halmashauri ya  Wilayani ya Mpanda  kilichofanyika  katika  ukumbi wa Idara  ya     Maji  kilichoongozwa  na  mwenyekiti wa  Halmashauri  hiyo Yassin Kiberiti
Katika kikao hicho  baadhi ya  madiwani  walimtaka   Mwenyekiti wao  wa Halmashauri hiyo  awape maelezo ya kina  kuhusiana  na  taarifa zilizoenea  kuwa   kuna mapendekezo  yamekuwa yakitolewa  kwenye  vikao mbalimbali yanayopingana  na uamuzi  wa  Baraza  la  Madiwani  la kuhamisha  ofisi za Makao yao makuu  na kuhamishia Kabungu
Diwani wa Kata ya Kabungu   Nassor  Kasonso  ndiye  aliyekuwa wa kwanza   kuhoji  na kutaka  kujua  ni  utaratibu upi ambao unataka kutumuka  kutengua  maamuzi yaliyopitishwa na Baraza  la  madiwani kwenye kikao chao Baraza  la   madiwani  walioamua  kuhamishia  makao  yao makuu  Kabungu na  badala yake   wahamii Katuma  Tarafafa  ya Mwese
Mwenyekiti wa Halmashauri  Yassin Kibiriti  alilieleza Baraza hilo  kuwa  ni kweli kuna  baadhi ya  vikao  vimekuwa  vikipendekeza  makao makuu   yahamishiwe   Kata ya Katuma  bila kuwashirikisha   madiwani ambao ndio  wenye      Halmashauri
Aliwafafanulia  maamuzi  ya  kikao cha   Baraza  la  madiwani kiliisha  amua  makao makuu yawe  Kabungu si kwinginepo   labda  kama   baraza hilo  litatengua uamuzi wao wa  ambao walikuwa wameutowa  hapo awali
Baraza  hilo la  madiwani  baada ya  kupata  maelezo ya  mwenyekiti wao wote kwa pamoja walipitisha  kwa kauli moja   uamuzi wao wa  kuhamishia  makao yao makuu Kabungu  uendelee kama ambavyo walivyokuwa wameamua  toka awali na sivinginevyo
Pia  katika  kikao hicho walijadili ombi  la SUMA JKT  ambao wameomba  wapatie  zaidi ya Ekari  5000 za  ardhi kwa  ajili ya  ujenzi a  kambi katika eneo la  Kijiji cha  Kamama  Kata ya  Mpanda  Ndogo
Madiwani hao  walishauri kuwa  kabla ya  ya Halmashauri  hiyo kuwapatia eneo hilo Suma JKT ni  vizuri kwanza   madiwani wakaenda kwenye  eneo hilo na kulikagua ili kuepukana na migogoro  ya ardhi ambayo inaweza kuja kujitokeza hapo baadaye

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa