Na Walter Mguluchuma
Mpanda Katavi
Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya
ya Mpanda Mkoa wa Katavi limepitisha uamuzi wa
kuhamisha Ofisi za Makao
yake makuu ya Halmashauri hiyo kutoka
Mjini Mpanda na
kuhamishia makao makuu yake
mapya katika Tarafa
ya Kabungu Wilayani
Uamuzi huo
ulitolewa hivi karibuni
katika kikao cha
Baraza la Madiwani la
Halmashauri ya Wilayani ya Mpanda kilichofanyika katika
ukumbi wa Idara ya Maji
kilichoongozwa na mwenyekiti wa
Halmashauri hiyo Yassin Kiberiti
Katika kikao
hicho baadhi ya madiwani
walimtaka Mwenyekiti wao wa Halmashauri hiyo awape maelezo ya kina kuhusiana
na taarifa zilizoenea kuwa
kuna mapendekezo yamekuwa
yakitolewa kwenye vikao mbalimbali yanayopingana na uamuzi
wa Baraza la
Madiwani la kuhamisha ofisi za Makao yao makuu na kuhamishia Kabungu
Diwani wa Kata ya
Kabungu Nassor Kasonso
ndiye aliyekuwa wa kwanza kuhoji
na kutaka kujua ni
utaratibu upi ambao unataka kutumuka
kutengua maamuzi yaliyopitishwa
na Baraza la madiwani kwenye kikao chao Baraza la
madiwani walioamua kuhamishia
makao yao makuu Kabungu na
badala yake wahamii Katuma Tarafafa
ya Mwese
Mwenyekiti wa
Halmashauri Yassin Kibiriti alilieleza Baraza hilo kuwa
ni kweli kuna baadhi ya vikao
vimekuwa vikipendekeza makao makuu
yahamishiwe Kata ya Katuma bila kuwashirikisha madiwani ambao ndio wenye
Halmashauri
Aliwafafanulia maamuzi
ya kikao cha Baraza
la madiwani kiliisha amua
makao makuu yawe Kabungu si
kwinginepo labda kama
baraza hilo litatengua uamuzi wao
wa ambao walikuwa wameutowa hapo awali
Baraza hilo la
madiwani baada ya kupata
maelezo ya mwenyekiti wao wote
kwa pamoja walipitisha kwa kauli
moja uamuzi wao wa kuhamishia
makao yao makuu Kabungu uendelee
kama ambavyo walivyokuwa wameamua toka
awali na sivinginevyo
Pia katika
kikao hicho walijadili ombi la
SUMA JKT ambao wameomba wapatie
zaidi ya Ekari 5000 za ardhi kwa
ajili ya ujenzi a kambi katika eneo la Kijiji cha
Kamama Kata ya Mpanda
Ndogo
Madiwani hao walishauri kuwa kabla ya
ya Halmashauri hiyo kuwapatia
eneo hilo Suma JKT ni vizuri kwanza madiwani wakaenda kwenye eneo hilo na kulikagua ili kuepukana na
migogoro ya ardhi ambayo inaweza kuja kujitokeza
hapo baadaye
No comments:
Post a Comment