Baadhi ya washiriki wa mkutano wa kongamano la uzinduzi rasmi wa mchakato wa uanzishwaji wa mfuko wa afya ya jamii tiba kwa kadi (TIKA) wakiwa kwenye mkutano uliofanyika jan kwenye Ukumbi wa Idara ya maji wakimsikiliza kwa makini mkuu wa mkoa wa katavi Dr. Rajabu Lutengwe ambaye hayupo pichani wakati akitoa hotuba ya uzinduzi rasmi wa mchakato wa uanzoshwaji wa mfuko wa jamii tiba kwa kadi.
Katibu wa chama cha walemavu Godfrey Sadala akichangia mawazo kwenye kikao cha wadau wa uzinduzi rasmi wa mchakato wa uanzishaji wa bima ya afya ya jamii tiba kwa kadi(TIKA) uliozinduliwa jana katika ukumbi wa Idara ya maji mjini mpanda na kuwashirikisha wadau mbalimbali, ambapo aliulizia namna ya walemavu watakavyonufaika na mfuko huo. Uzinduzi huo rasmi uliwashirkisha wadau mbalimbali wa mji wa mpanda na kupokewa kwa furaha na washiriki wa kongamano hilo ambapo mgeni rasmi alikuwa mkuu wa mkoa wa Katavi Dr. Rajabu Lutengwe.
Picha na Walter Mguluchuma
Na Walter Mguluchuma
Mpanda Katavi
Mkuu wa Mkoa wa Katavi DR Rajabu Rutengwe amezindua Rasmi mchakato wa uanzishwaji wa Mfuko wa Afya ya Jamii ya Tiba kwa njia ya kadi TIKA katika Halmashauri ya Mji wa Mpanda Mkoa wa Katavi
Uzinduzi huo ulifanyika hapo jana katika ukumbi wa Idara ya maji ambapo ndio ilikuwa ni siku ya wadau wa Mji wa Mpanda
Mkuu wa Mkoa Dr Rutengwe katika hotuba yake ya ufunguzi kwa wadau wa mchakato wa uanzishwaji wa sheria ndogo na hati rasmi ya mfuko wa Afya ya Jamii kwa kadi kwa mji Mpanda aliwataka wadau watambue umuhimu wa mpango wa uchangiaji kabla ya kuugua
Alisema ni vizuri wadau wakaharakisha kupitisha mchakato huo wa kutunga sheria ndogo ili ianze kutumika kwa wananchi wa Mji wa Mpanda na waweze kunufaika na mfuko huo kama ambavyo wanavyo nufaika watu wa Miji mingine wanao tumia mfuko huo
Alieleza mpango kwa Tiba kwa kadi utakuwa na manufaa kwa wakazi wa Mji wa Mpanda kwani mpango huo ni mzuri na hasa kwa watu wenye kipato kidogo kwa kuchangia kiasi cha shilingi elfu kumi kwa mtu mmoja kwa mwaka mzima na kiasi hicho kinamfanya mchangiaji apate matibabu kwa kipindi cha mwaka mzima
Aidha aliutaka Mfuko wa Bima ya Afya NHIF iandae utaratibu mzuri wa kuweka kumbukumbu za wanachama wa TIKA na wawe na mpango endelevu wa kutoa elimu mara kwa mara kwa makundi mbalimbali ili kuwahamasisha wajiunge na mfuko wa TIKA
Pia aliiangiza Halmashauri ya mji wa Mpanda kuhakikisha asilimia 67 ya fedha zinazo patikana zinanunuliwa ndawa kwani haitakuwa vema fedha hizo wakazitumia kwa wanufaa mwngine na kusababisha wanachama kukosa dawa pindi waunguapo na matokeo yake wanaweza wakasababisha watu wakauchukia mfuko huo pasipo na sababu
Alisema iandae utaratibu wa kuzijua familia ambazo zina hari hari ngumu kiuchumi ambazo zinashindwa kuchangia katika mpango huu na wakisha zitambua Halmashauri iweke utaratibu wa kuzichangia familia hizo kwani hari ya upatikanaji wa dawa katika hospitali na kwenye vituo vya Afya na zahati katika Mkoa wa Katavi sio wakuridhisha
Kwa upande wake mwakilishi wa wa kaimu Mkurugenzi wa wa Mfuko wa Bima ya Afya NHIF Celestini Muganga alieleza kuwa jumla ya Halmashauri 128 zilizopo hapa nchini zinanufaika na mfuko huo kati ya Halmashauri 168 zilizopo hapa nchini
Alisema lengo la mfuko huo ni kuhakikisha wanachama wake hawakosi dawa pindi wanapo kuwa wameugua na ndio maana mfuko huo umeweka utaratibu wa kuzikopesha fedha Halmashauri kwa ajiri ya kununulia dawa na pia wanatowa zaidi kwa Halmashauri ambayo iliyoongoza kwa kuingiza wanachama wappya
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Paza Mwamlima alisema ipotabia kwa baadhi ya watumishi wa idara ya Afya kuwanyanyasa watu wanakwenda kutibiwa kwenye hospitali vituo vya afa na Zahanati kwa kutumia kadi
Wil aya ya Mpanda ni miongoni mwa Halmashauri 40 hapa nchini ambazo zilikuwa hazijajiunga na mfuko wa wa Af ya ya Bima ya jamii TIKA na hari ambayo ilisababisha wakazi wa mji huu kukosa huduma hii muhimu
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
No comments:
Post a Comment