Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
jela miaka 30 kwa
kubaka kikongwe
N a Walter Mguluchuma
Mpanda Katavi
Mahakama ya Wilaya ya Mpanda
Mkoa wa Katavi imemuhukumu
John Joseph 30
Mkazi wa Tarafa ya M pibwe Wilaya
ya Mlele Mkoani hapa kifungo cha miaka 30 jela baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka kwa nguvu kikongwe mwenye umri wa
miaka 65
Hukumu hiyo ilitolewa
hapo juzi na Hakimu Mkazi Mfawidhiwa
Mahakama ya Wilaya ya Wilaya ya Mpanda
Chiganga Ntengwa baada ya mahakama
kulidhika na ushahidi uliotolewa mahakamani na kuvutia hisia za watu wengi
Awali katika kesi hiyo
mwendesha mashitaka Godfrey Luzabila
alidai mahakamani hapo kuwa mshitakiwa alitenda kosa hilo hapo Agosti 18
mwaka jana majira ya saa 12 jioni katika
eneo la kijiji cha Ifukutwa Tarafa ya Kabungu wilayani Mpanda ambako
mshitakiwa alikuwa amekwenda kufanya kazi za kibarua cha
kutengeneza barabara
Anadaiwa siku
hiyo alimwona mama huyo akiwa akipita
barabarani na ndipo mshitakiwa alimfuata
mama huyo na kumvutia kwenye kichaka
pembeni ya barabara aliyokuwa
akifanya kazi mshitakiwa ya kuchimba mitaro
Mwendesha mashitaka Godfrey
aliiambia mahakama mshitakiwa
baada ya kumvutia kikongwe huyo polini
alimtaka afanye nae tendo la ndoo
kitendo ambacho mama huyo
hakukubaliana nacho
Alisema mama huyo alimsihi
mshitakiwa akatafute mwanamke
mwingine wa kufanya nae tendo la ndoa
kwani umri wake haulingani kabisa na
umri wa mshitakiwa John Joseph
Alisema pamoja na
maombi ya mama huyo mshitakiwa hakujali na ndipo alipomshika mama huyo
na kumvua nguo kwa nguvu na kuanza kumbaka huku mama huyo akipiga mayowe ya kuomba msaada
Mwendesha mashitaka alisema
kufuatia mama huyo kupiga mayowe
watuu watatu waliokuwa wakipita kwenye eneo hilo waliweza kusikia
na waliweza kwenda kichakani na walimwona mshitakiwa akiwa akimbaka mama huyo na kasha mshitakiwa alivyo ona wanamsogelea
alitokomea kichakani mahari kusiko julikana
Hakimu Mkazi
mfawidhi Chiganga Ntengwa akisoma
hukumu hiyo alieleza kuwa
kutokana na ushahidi uliotolewa na
upande wa mashitaka ambao ulileta mashahidi watatu akiiwepo wa
daktari ambae alithibiitisha kuwa mama huyo alikuwa amebakwa na kuharibiwa
sehemu za siri hivyo mahakama haikuona
shaka lolote kumtia mshitakiwa hatiani
Hivyo mahakama imemtia mshitakiwa hatiani kwa kosa la
kifungu cha sheria namba 130 kifungu kidogo cha kwanza na chapili na
kifungu cha sheria namba 131
Alisema kutokana na
kupatikana na makosa hayo mahakama
imemuhukumu mshitakiwa John Joseph
kutumikia kifungo cha miaka 30
kuanzia hapo juzi
0 comments:
Post a Comment