Na Walter Mguluchuma
Mpanda Katavi
Watu watatu Raia wa Nchi ya Vetnam wamefikishwa kizimbani kwenye Mahakama ya Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi kwa tuhuma za kuingia kwenye Makazi ya Wakimbizi ya Katumba Wilaya ya Mlele Mkoani hapa
Raia hao wa Nchi yaVetnam waliofikishwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya ya Mpanda mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahama ya Wilaya ya Mpanda Chiganga Ntengwa
Waliofikishwa kizimbani kwa tuhuma za kuingia kwenye makazi ya Wakimbizi ya Katumba ni Chuqup Ngtun 29,Phamnquyen Huyadang 34 na Tran Huum 29 wote raia wa Nchi ya Vetnam
Mwendesha mashitaka Mkaguzi wa Polisi Ally Mbwijo alidai Mahakamani hapo kuwa watuhumiwa hao walitenda kosa hilo hapo machi 21 majira ya saa tano asubuhi
Alidai kuwa siku hiyo ya tukio Raia hao watatu wa Nchi ya Vetnam walikamatwa wakiwa kwenye Kijiji cha Tambazi kilichoko katika makazi ya wakimbizi ya Katumba Wilayani Mlele wakiwa wameingia ndani ya Makazi hayo bila kuwa na kibali
Washitakiwa wanadaiwa kuwa baada ya kukamatwa na walipohojiwa walidai kuwa wao ni waandisi wa maswala ya mawasiliano na waliingia kwenye makazi hayo kwa ajiri ya kufanya shughuli ya mawasilano ya mitandao mbalimbali
Washitakiwa hao watatu Raia wa Vetnam baada ya kusomewa mashitaka hayo na mwendesha Mashita walikana mashitaka hayo ambayo walisomewa mahakamani hapo
Hakimu Mkazi Mawidhi Chiganga Ntengwa aliamuru washitakiwa kwenda mahabusu katika Gereza la Mpanda mjini hadi hapo machi 25 baada ya washitakiwa kukosa watu wa kuwadhamini licha ya mdhamana wao kuwa wazi
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment