Na Walter Mguluchuma
Mpanda Katavi
Hospitali ya
Wilaya ya Mpanda inakabiliwa na tatozo la upungufu wa madawa mbalimbali ya kuwatibia Binadamu
kutokana na Hospitali
hiyo kutowa huduma ya kuwahudumia
wakazi wote wa Mkoa wa Katavi huku Halmashauri zilizopo
Mkoani hapa zikiwa
zimeshindwa kuchangia fedha za ununuzi
wa dawa licha ya wakazi wa Halmashauri
zao kupatiwa huduma katika Hospitali
hiyo
Haya yalisemwa
hapo jana kwenye kikao cha Baraza la
madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda kilichofanyika katika ukumbi
wa Maji
na mganga Mkuu wa Wiliya ya Mpanda Dr Joseph Msemwa
Dr Msemwa alilieleza Baraza la Madiwani kuwa Hospitali ya Wilaya
ya Mpanda inakabiliwa na changamoto ya
upungufu wa dawa za Binadamu kutokana
na Hospitali hiyo kumiwa na wakazi wote
wa Halmashauri za Mkoa huu kupatiwa
huduma na Hospitali hiyo
Aliwaeleza Madiwani kuwa
licha ya Halmashauri hizo wananchi wake kupatiwa huduma hapo
zimekuwa zikiombwa zichangie
kununua dawa lakini zimeshindwa
kufanya hivyo na matokeo yake mzogo wote wa kuihudumiaHospitali hiyo imeachiwa
Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda peke yake licha ya kuhudumia Mkoa mzima wa Mkoa
wa Katavi
Dr Msemwa
alifafanua kutokana na kuelemewa
kwa Hospitali hiyo ndio maana walikuwa wameomba Hospitali hiyo ipandishwe hadhi na kuwa Hospitali ya Mkoa wa Katavi
lakini ilishindikana kutokana na kukosa
vigezo
Mganga mkuu huyo
wa Wilaya alilazimika kutowa maelezo
hayo kufutia madiwani wawili Diwani
Nassor Kasonso wa Kata ya Kabungu na Thiodela Kisesa wa viti maalumu
kutaka yatolewe maelezo ya kina kinachosababisha Hospitali hiyo kuwa
na tatizo la upungufu wa dawa za mara kwa mara
Pia Diwani Kasonso
aliishauri Halmashauri hiyo kuwa na
utaratibu wa kuwafanya mawakala wanaofanya shughuli za kukusanya
ushuru wawe wanapewa barua ya kuwatambulisha madiwani kwenye eneo
usika tofauti na ilivyo
sasa ambapo mawakala wanaokusanya ushuru
hata Diwani wa kata husika wanakuwa
hawafamiani
Kwaupande wake
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda Justine Tibenderana alikiri
kuwepo kwa tatizo la mawakala
kutofahamika kwa madiwani wa kata husika hivyo Halmashauri inaandaa utaratibu
wa kuwa wanawaandikia barua madiwani za
kuwatambulisha wakala husika na wakala kabla ya kuanza shughuli atalazimika kulipoti kwa Diwani wa eneo
0 comments:
Post a Comment