Monday, March 24, 2014

RAIA WATATU WA VIETNAM KIZIMBANI KWA KUINGIA KWENYE MAKAZI YA WAKIMBIZI BILA KIBALI

Na  Walter Mguluchuma
Mpanda  Katavi
Watu watatu Raia wa Nchi ya Vetnam wamefikishwa  kizimbani  kwenye Mahakama ya Wilaya ya Mpanda  Mkoa wa Katavi kwa tuhuma za kuingia kwenye Makazi ya Wakimbizi ya Katumba  Wilaya ya Mlele Mkoani hapa
Raia hao wa Nchi yaVetnam waliofikishwa  kizimbani  katika Mahakama ya Wilaya ya Mpanda mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahama ya Wilaya ya Mpanda Chiganga Ntengwa
Waliofikishwa kizimbani kwa tuhuma za kuingia kwenye makazi ya Wakimbizi ya Katumba ni Chuqup Ngtun 29,Phamnquyen Huyadang 34 na  Tran Huum 29 wote raia wa Nchi ya Vetnam
Mwendesha mashitaka Mkaguzi wa  Polisi Ally Mbwijo alidai Mahakamani  hapo  kuwa watuhumiwa  hao walitenda kosa hilo hapo machi  21 majira ya saa tano asubuhi
Alidai kuwa siku hiyo ya tukio Raia hao watatu wa Nchi ya Vetnam  walikamatwa wakiwa kwenye Kijiji cha Tambazi  kilichoko katika  makazi ya wakimbizi ya Katumba  Wilayani Mlele  wakiwa wameingia ndani ya Makazi hayo bila kuwa na kibali
Washitakiwa wanadaiwa kuwa baada ya kukamatwa  na walipohojiwa walidai kuwa wao ni  waandisi wa maswala ya mawasiliano na waliingia kwenye makazi hayo kwa ajiri ya kufanya shughuli ya mawasilano ya mitandao mbalimbali
Washitakiwa hao watatu Raia wa Vetnam  baada ya kusomewa mashitaka hayo  na mwendesha Mashita walikana mashitaka hayo  ambayo walisomewa mahakamani hapo

Hakimu Mkazi  Mawidhi Chiganga Ntengwa aliamuru washitakiwa  kwenda mahabusu katika Gereza la Mpanda  mjini hadi hapo  machi 25 baada ya washitakiwa  kukosa watu wa kuwadhamini licha ya mdhamana wao kuwa wazi 
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

No comments:

Post a Comment