Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
N a Walter
Mguluchuma
Waziri Mkuu Mizengo
Pinda ameziagiza Halmashauri zote hapa Nchini kuweka mipango
ya utaratibu wa kuendeleza ufugaji wa nyuki ili kuwawezesha na
kuwasaidia wananchi kuongeza kipato chao
Agizo hilo
alilitowa hapo juzi wakati wa maadhimisho ya siku ya utundikaji wa
mizinga ya asali yaliyofanyika Kitaifa katika Tarafa ya Inyonga Wilayani Mlele
Mkoa wa Katavi katika hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na Waziri wa
Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu
Alisema mahitaji ya
asali yameongezeka sana Duniani kwa sasa hivyo wakurungezi wa Halmashauri
zote hapa N chini waakikishe wanaweka mipango ya utaribu wa
kuendeleza ufugaji wa nyuki ili kuweza kumwongezea mwananchi kipato
na pato la Taifa kwa ujumla
Alizitaka
Halmashauri zote hapa Nchini zihakikishe zinatenga bajeti kwenye Halmashauri
zao kwa ajiri ya wafugaji nyuki katika maeneo yao
Alisema Serikali
imeweka mkakati wa kuimalisha mbinu bora za ufugaji wa
nyuki ili kuwafanya wafugaji wa nyuki kupata asali bora na
kujiongezea kipato chao
Alifafanua kuwa hivi
sasa wafugaji wengi wa nyuki ni wazee ila sasahivi ufugaji umeboreshwa
hivyo hata wanawake wajitokeze kwa wingi kufanya shughuli
hiyo ya ufugaaji wa nyuki
Pia aliitaka Wizara
itenge maeneo kwa ajiri ya kuhifadhi mazingira
kwa ajiri ya kuhifadhi nyuki ili kuwepo kwa nyuki wa
kutosha
Kwa upande wake
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na utalii Maimuna Tarishi alisema lengo la
Wizara ni kuhahakikisha uzalishaji wa asali unaongezeka kwa
asilimia 50 katika kipindi miaka mitano ijayo kwani
uzalishaji wa asali kwa sasa tani 1,338,000
Alisema kataka
kuendea kuhamasisha ufugaji wa nyuki Serikali imeandaa kongamano la
la kimataifa litakalo fanyika Mkoani Arusha mwezi Novemba mwaka
huu lenye lengo la kuhamasisha ufugaji wa nyuki wa kisasa
Kwa upande wake Mkuu
wa Mkoa wa Katavi Dr Rajabu Rutengea alisema mkoa wa Katavi ni miongoni mwa
mikoa yenye msitu mikubwa ya miombo ambayo inawasaidia wafugaji
kujipatia kipato chao ambapo mkoa wa Katavi msimu uliopita ulizalisha
tani 8,518 za asali
No comments:
Post a Comment