Monday, March 17, 2014

WILAYA YA MPANDA YATEKELEZA MIRADI YA MAJI KWA ASILIMIA 70

N a  Walter Mguluchuma
Mpanda Katavi
Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi  imefanikiwa  kutekelezaji wa miradi ya maji  kwa zaidi ya asilimia 70 yenye thamani ya pesa  shilingi Bilioni  2. katika msimu wa fedha wa  mwaka 2013 na 2014-03-17
Hayo yalisemwa  hapo juzi na  Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda  Justine Tibenderana  wakati wa  maadhimisho  ya  ufunguzi  wa wiki ya  maji   katika Wilaya ya mpanda  yaliofanyika  katika  Kijiji cha Karema   Wilayani Mpanda
Alisema hadi sasa  katika msimu wa fedha wa mwaka 2013 na 2014  Wilaya ya Mpanda  imefanikiwa  kutekeleza  zaidi ya asilimia  70 ya miradi ilipangwa  yenye  thamabi ya shilingi  Bilioni  Tsh 2,611,924,319
Tibenderana aliitaja miradi hiyo  kuwa ni ujenzi wa  mfumo wa maji  ya bomba  katika kijiji cha Karema  ujenzi wa mfumo wa maji  ya bomba katika Kijiji  cha Milala , ujenzi wa visima vifupi katika vijiji vya  Itunya  Kakese,  Mnyagala,
Aliitaja miradi mingine kuwa  ni uchimbaji wa visima  virefu katika vijiji vya  Isenga,Ikaka  na  ujenzi wa visima virefu katika kaijiji cha Katuma  na ujenzi  wa mradi wa maji  ya mseleleko  katika kijiji cha Mwese  pamoja na na  upanuzi wa mradi wa   maji  ya bomba  kutoka kijiji cha Karema  hadi Kijiji cha Itetenya
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Paza Mwamlila ambaealikuwa  mgeni  rasimi wa ufunguzi wa maadhimisho   hayo  alisema  Serikali ya Wilaya ya Mpanda inatambua    tatizo kubwa la maji katika Kata ya Karema  ambalo kwa kiasi kikubwa  wakazi wa kata hiyo  wamekuwa wakipatwa na  milipuko ya ya magonjwa  kila mwaka
Alisema Wilaya ya Mpanda inakabiliwa na  na changamoto   kubwa  ya upatikanaji wa huduma ya maji  kwani mpaka sasa  ni asilimia 48  tu ya wa wananchi wa   Wilaya ya Mpanda wanao  huduma ya maji safi na salama
Mwamlima alitaja changamoto nyingine kuwa ni  uharibifu wa  vyanzo vya  maji  na uhamiaji  mkubwa  wa wananchi wanao  mikoa ya jirani  ya Kigoma  Mwanza , Tabora na Shinyanga  ambao wahamiaji hao  wamekuwa wakifanya  wakifanya shughuli za kibinadamu kwenye  vyanzo vya maji  na kupelekea  kupungua na hata kukauka kwa vyanzo vya maji
Nao  wakazi wa kata hiyo ya Karema katika risara yao iliyosomwa na Joseph Lusambo mbele ya mkuu wa Wilaya ya Mpanda  waliilalamikia  kampuni ya  GEOFFSON INVESTTIMENT LTD ya Deres salaam  kwa kushindwa kukamilisha waujenzi wa  mradi wa maji unao dhaminiwa  na Benki  ya Dunia kwa thamani ya shilingi milioni 342.701.165

Mradi huo ulinza kujengwa   june mwaka jana  na  ulitakiwa ukamilike Desemba mwaka jana  ambapo shughili hizo za ujenzi  wa tanki  nyumba ya kuhifadhi mashine na usambazaji wa bomba umesimama 
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

No comments:

Post a Comment