N a Walter Mguluchuma
Mpanda Katavi
Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi imefanikiwa kutekelezaji wa miradi ya maji kwa zaidi ya asilimia 70 yenye thamani ya pesa shilingi Bilioni 2. katika msimu wa fedha wa mwaka 2013 na 2014-03-17
Hayo yalisemwa hapo juzi na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda Justine Tibenderana wakati wa maadhimisho ya ufunguzi wa wiki ya maji katika Wilaya ya mpanda yaliofanyika katika Kijiji cha Karema Wilayani Mpanda
Alisema hadi sasa katika msimu wa fedha wa mwaka 2013 na 2014 Wilaya ya Mpanda imefanikiwa kutekeleza zaidi ya asilimia 70 ya miradi ilipangwa yenye thamabi ya shilingi Bilioni Tsh 2,611,924,319
Tibenderana aliitaja miradi hiyo kuwa ni ujenzi wa mfumo wa maji ya bomba katika kijiji cha Karema ujenzi wa mfumo wa maji ya bomba katika Kijiji cha Milala , ujenzi wa visima vifupi katika vijiji vya Itunya Kakese, Mnyagala,
Aliitaja miradi mingine kuwa ni uchimbaji wa visima virefu katika vijiji vya Isenga,Ikaka na ujenzi wa visima virefu katika kaijiji cha Katuma na ujenzi wa mradi wa maji ya mseleleko katika kijiji cha Mwese pamoja na na upanuzi wa mradi wa maji ya bomba kutoka kijiji cha Karema hadi Kijiji cha Itetenya
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Paza Mwamlila ambaealikuwa mgeni rasimi wa ufunguzi wa maadhimisho hayo alisema Serikali ya Wilaya ya Mpanda inatambua tatizo kubwa la maji katika Kata ya Karema ambalo kwa kiasi kikubwa wakazi wa kata hiyo wamekuwa wakipatwa na milipuko ya ya magonjwa kila mwaka
Alisema Wilaya ya Mpanda inakabiliwa na na changamoto kubwa ya upatikanaji wa huduma ya maji kwani mpaka sasa ni asilimia 48 tu ya wa wananchi wa Wilaya ya Mpanda wanao huduma ya maji safi na salama
Mwamlima alitaja changamoto nyingine kuwa ni uharibifu wa vyanzo vya maji na uhamiaji mkubwa wa wananchi wanao mikoa ya jirani ya Kigoma Mwanza , Tabora na Shinyanga ambao wahamiaji hao wamekuwa wakifanya wakifanya shughuli za kibinadamu kwenye vyanzo vya maji na kupelekea kupungua na hata kukauka kwa vyanzo vya maji
Nao wakazi wa kata hiyo ya Karema katika risara yao iliyosomwa na Joseph Lusambo mbele ya mkuu wa Wilaya ya Mpanda waliilalamikia kampuni ya GEOFFSON INVESTTIMENT LTD ya Deres salaam kwa kushindwa kukamilisha waujenzi wa mradi wa maji unao dhaminiwa na Benki ya Dunia kwa thamani ya shilingi milioni 342.701.165
Mradi huo ulinza kujengwa june mwaka jana na ulitakiwa ukamilike Desemba mwaka jana ambapo shughili hizo za ujenzi wa tanki nyumba ya kuhifadhi mashine na usambazaji wa bomba umesimama
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment