Home » » Pinda Agiza Halmashauri kuweka mipango ya kuendeleza ufugaji wa nyuki

Pinda Agiza Halmashauri kuweka mipango ya kuendeleza ufugaji wa nyuki

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

N a Walter Mguluchuma 

Waziri Mkuu Mizengo Pinda ameziagiza  Halmashauri zote hapa Nchini  kuweka  mipango ya utaratibu wa kuendeleza  ufugaji wa nyuki  ili kuwawezesha na kuwasaidia wananchi  kuongeza kipato chao 

Agizo  hilo  alilitowa hapo juzi  wakati wa maadhimisho ya siku ya utundikaji wa mizinga ya asali yaliyofanyika Kitaifa katika Tarafa ya Inyonga Wilayani Mlele Mkoa wa Katavi  katika hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu 
Alisema mahitaji ya asali yameongezeka sana   Duniani kwa sasa hivyo wakurungezi wa Halmashauri zote hapa  N chini  waakikishe wanaweka  mipango ya utaribu wa kuendeleza  ufugaji wa nyuki  ili kuweza kumwongezea mwananchi kipato na pato la Taifa kwa ujumla 

 Alizitaka Halmashauri zote hapa Nchini zihakikishe zinatenga bajeti kwenye Halmashauri zao kwa ajiri ya wafugaji nyuki katika maeneo yao 

Alisema Serikali imeweka  mkakati  wa kuimalisha  mbinu bora  za ufugaji wa nyuki  ili kuwafanya wafugaji wa nyuki kupata asali bora  na kujiongezea kipato chao

Alifafanua kuwa hivi sasa wafugaji wengi wa nyuki ni wazee  ila sasahivi ufugaji umeboreshwa  hivyo hata wanawake  wajitokeze  kwa wingi kufanya shughuli hiyo ya ufugaaji wa nyuki 

Pia aliitaka Wizara   itenge  maeneo  kwa ajiri  ya kuhifadhi  mazingira  kwa ajiri ya  kuhifadhi nyuki  ili kuwepo kwa nyuki wa kutosha 

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na utalii Maimuna Tarishi alisema lengo la Wizara  ni kuhahakikisha  uzalishaji wa asali unaongezeka kwa asilimia 50 katika kipindi  miaka mitano  ijayo  kwani uzalishaji wa asali kwa sasa  tani  1,338,000

Alisema kataka kuendea kuhamasisha ufugaji wa nyuki Serikali imeandaa  kongamano la  la kimataifa   litakalo fanyika Mkoani Arusha mwezi Novemba mwaka huu lenye lengo la kuhamasisha ufugaji wa nyuki wa kisasa

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dr Rajabu Rutengea alisema mkoa wa Katavi ni miongoni mwa mikoa yenye msitu  mikubwa ya miombo  ambayo inawasaidia wafugaji kujipatia kipato chao  ambapo mkoa wa Katavi msimu uliopita ulizalisha  tani 8,518 za asali 
 

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa