Home » » AUWA KWA KIPIGWA NA KITU KIZITO KICHWANI BAADA YA KUWATISHIA WANAKIJIJI UCHAWI‏

AUWA KWA KIPIGWA NA KITU KIZITO KICHWANI BAADA YA KUWATISHIA WANAKIJIJI UCHAWI‏

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Na  Walter Mguluchuma
Mpanda Katavi
Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Kalenga  Mashaka  52  Mkazi  wa Kijiji  cha Kusi makazi ya wakimbizi yamishamo
  Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi  ameuwawa  kwa kupigwa  na kitu  kizito  kichwani  na watu wasiojulikana
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi kamishina Maidizi Mwandamizi Dhahiri Kidavashari   tukio hilo lilitokea hapo juzi majira ya saa mbili asubuhi kijijini  hapo
Alisema katika uhai wake marehemu  aliwahi  kufikishwa  katika uhai  wake marehemu  aliwahi kufikishwa  katika mahakama ya mwanzo ya Mishamo  kwa kutuhumiwa  kutishia kuuwa  kwa maneno ambapo alikuwa  akiwatishia watu  kuwauwa  kwa njia ya ushirikina
Kamanda Kidavashari alifafanua kuwa kitendo hicho cha kuwatishia wakazi wa kijiji  hicho  kwa njia ya ushirikina kilijenga chuki baina ya marehemu na wanakijiji hicho
Alifafanua kuwa  kwa  mujibu wa uchunguzi wa  awali   chanzo   hicho kutishia   kuwauwa kwa ushirikina wanakijiji wenzake  ndicho kilichosababisha kutokea kwa mauwaji ya mtu hoyo
Alisema kuwa  wanakijiji  hicho cha Kusi  walikuwa wamechoshwa na vitendo hivyo  vya kutishiwa kuondolewa uhai wao kwa njia ya ushirikina alivyokuwa akivifanya marehemu  Kalenga
Kidavashari  alieleza  kabla ya tukio la marehemu    kufikishwa  kwenye mahakama ya mwanzo ya Mishamo  wanakijiji hicho  waliwahi kujichukulia   sheria  mkononi  kwa kuichoma moto nyumba ya marehemu  kwa lengo la  kumfukuza kijini hapo
Polesi wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo  ili kuwabaini watu au mtu aliyehusika na mauwaji hayo ili  waweze kufikishwa kwenye vyombo vya sheria

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa