Na Walter
Mguluchuma
Mpanda
Katavi
Aliyekuwa
mgombea nafasi ya Mwenyekiti wa
Taifa katika uchaguzi
wa chama cha NCCR MAGEUZI katika
uchaguzi ulipita mwishoni mwa mwaka
jana aliyegombea na Jemes Mbatia Charles Makofila amefariki dunia
usiku wa kuamkia jana katika kijiji cha Mpandandogo Tarafa ya Kabungu
Kwa mujibu wa
taarifa kutoka kwa mjomba wake Hamadi
Mapengo ambae ni Diwani wa Kata ya
Mpanda ndogo alisema marehemu alifariki majira ya saa nane
usiku wa kuamkia jana
Alisema marehemu
alifariki akiwa nyumbani kwake kutokana
na maradhi ya ugojwa wa homa ya matumbo ambapo umeugua zaidi ya mwezi mmoja na alikuwa akitibiwa katika zahanati ya
kijiji hicho
Katika uhai
wake marehemu aliwahi kuwa kiongozi wa
chama hicho ambapo
mpaka anafariki Dunia allikuwa ni
Kamishina wa mkoa wa Katavi
Pia mbali ya kugombea na Jemes Mbatia nafasi ya uwenyekiti wa Taifa
wa chama hicho marehemu aliwahi kuwa mgombea wa ubunge wa jimbo la Mpanda Vijijini kupitia
chama hicho katika uchaguzi mkuu wa
mwaka 2010
Mjomba huyo wa marehemu
alieleza kuwa marehemu Charles Makofila
atazikwa leo kwenye mababuri ya kijiji cha Mpanda ndogo majira ya saa
nane mchana
0 comments:
Post a Comment