Home » » KIKONGWE AKUTWA AMEUAWA CHUMBANI KWAKE KWA KUKATWA MAPANGA

KIKONGWE AKUTWA AMEUAWA CHUMBANI KWAKE KWA KUKATWA MAPANGA

Na  Walter  Mguluchuma
Mpanda Katavi
Mtu mmoja Shoma  Salumu  (78)  Mkazi wa Kata ya Kakese Mkwajuni Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi amekutwa akiwa ameuwawa kwenye chumba chake kwa kukatwa  mapanga sehamu  za kichwani  na juu ya sikio na watu wasiojulikana

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi  wa Mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashari tukio hilo la mauwaji hayo  lilitokea hapo Desemba 29 majira ya saa mbili na nusu asubuhi  kijijini hapo nyumbani kwa motto wa marehemu aitwaye  Lameck Mboka

Alisema  siku moja kabla ya tukio hilo hapo majira ya saa saba mchana  marehemu akiwa  katika shughuli zake  za kila siku za kufinyanga vyungu na uganga wa kienyeji kwenye mji wa  Magdarena  Mhoja  walifika  vijana wawili  waliotambulika kwa majina ya  Shigera   Majinja  (25) na  Mhoja  Shilinde (18) wakazi wa kijiji hicho  ambao walijifanya ni wateja wake wa vyungu na kwa ajiri ya matibabu ya tiba za jadi

Alieleza ndipo walipoanza kumhoji marehemu  juu ya mambo mbalimbali ikiwa ni  pamoja na kutaka kujua  mahari ambapo marehemu alikokuwa akiishi  na chumba  alichokuwa  akilala  na alikuwa akilala na nani

Marehemu  aliwajibu watu hao  kwa ufasaha bila kuwa na mashaka nao huku mazungumzo hayo yakiwa  yanasikilizwa na Tausi  Mlitoni  ambae nae alikuwa kwenye eneo hilo akiwa shahidi wa  mazungumzo hayo

 Ailesama ndipo siku hiyo ya desemba 29  majira ya saa mbili na nusu asubuhi   mke wa Lameck Mboka  Zamda  Militone baada ya kuona  mama mkwe  amechelewa kuamka  alienda  kujaribu kufungua mlango  na kukuta umefungwa  kwa nje 

Kidavashari alieleza ndipo  Zamda alipofungua mlango huo wa chumba cha mama mkwe wake na kuingia ndani  na alimkuta mama mkwe wake  akiwa ameuwawa kinyama kwa kukatwa  mapanga  kicwani na kwenye siko la lake kulia

Baada ya kuona hari hiyo ya mauwaji ya kinyama alipiga mayowe  na majirani walifika kwenye eneo hilo la tukio na kujionea jinsi marehemu alivyokuwa ameuwawa kinyama

Kamanda Kidavashari alisema jeshi la polisi linawashikilia watu watatu kuhusiana na tukio hilo ambao ni  Shigera  Majija (26)   Mhoja Shilinde (18)   na  Masanja Ngasa (31) wakazi wa kijiji hicho cha Kakese na mtuhumiwa wanee  Walu  Ngasa bado anaendelea kutafutwa na polisi baada ya kukimbia 

Kwa mmijibu wa Kidavashari   watuhumiwa hao  wanatarajiwa kufikishwa mahakamani  baada ya upelelezi wa tukio hilo utakapo kuwa umekamilika

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa