Home » » MWANAMKE AUAWA KWA KUKATWA NA PANGA BAADA YA KUKATAA KUISHI NA MUMEWE

MWANAMKE AUAWA KWA KUKATWA NA PANGA BAADA YA KUKATAA KUISHI NA MUMEWE

Na walter Mguluchma
Mpanda,Katavi

MKAZI wa   kitongoji  cha Tulieni kata ya Itenka  wilayani  Mlele, Rehema  Lubinza (47) ameuawa  kikatili  kwa  kucharangwa  na mapanga na mumewe  kisha  mwili  wake  kufungiwa  ndani  ya nyumba   kwa  siku  tatu.

 Kamanda  wa Polisi Mkoa  wa Katavi , Kamishina Dhahiri Kidavashari  amethibitisha kutokea  kwa tukio hilo  lililotokea  siku ya mkesha wa  Sikukuu ya Krismasi , Desemba 24  usiku  katika kitongoji  hicho  cha Tulieni  wilyani Mlele  .

Kidavashari  alimtaja  mtuhumiwa  huyo wa mauaji kuwa  Mathis Mashini “Igoka’ (46)  mkazi  wa kitongoji  cha kijiji  hicho  cha Tulieni  ambaye  ndie  mume wa marehemu ..

Kwa mujibu  wa  Kamishina Kidavashari  alidai kuwa  kwa siku  kadhaa  wanandoa hao  walikuwa    wakishutumiana  ambapo  mke alikuwa  akimshutumu  mumewe  kwa kushindwa kumpatia  mahitaji  muhimu  ukiwemo  unyumba kwa muda mrefu .

Inadaiwa kuwa  baada  ya  kuoana miaka kadha iliyopita  ,  mke  ambaye  tayari  alikuwa ameshajijengea  nyumba  ya kuishi alimkaribisha mumewe  huyo  ambapo  walikuwa  wakiishi i  pamoja  katika  nyumba  hiyo ya  mwanamke huyo  iliyopo  katika kitongoji  hicho  cha Tulieni.

Kwa mujibu  wa Kidavashari ,   mke  alimtaka  mumewe  huyo   atoke  nyumbani  kwake (Rehema)  hapo   kwa  madai  kuwa  ameshindwa  kumpatia matumizi muhimu  ukiwemo unyumba  kwa muda mrefu  kauli ambazo  zilimkasirisha mume  huyo ambaye  inadaiwa hakuwa  tayari  kuachana na  mkewe  huyo .

Inaidaiwa mwanamke  huyo  alimfukuza mumewe huyo nyumba  hapo  akisisitiza lazima aondoke  ndipo  mume huyo  akishirikiana na  mkazi wa  kitongoji  hiyo  aliyetambuliwa  kuwa  Ngussa Masengwa (39)  walimshambulia  mwanamke huyo  kwa mapanga  akiwa amelala  nyumbani  kwake hapo   na kumjeruhi vibaya sehemu  mbalimbali  ya mwili wake na kumsababishia umauti   kisha  waliufungia mwili  wa marehemu  ndani ya  nyumba yake hiyo . .

Kwa mujibu  wa  Kidavashari  Siku ya Desemba 25  majirani  baada  ya kutowaona  wanandoa hao   huku nyumba yao  ikiwa imefungwa  mchana  kutwa, waliamua kuwasiliana  na Mthias  kwa  simu  yake ya mkononi  ambaye  aliwaeleza kuwa  wako  Mpanda mjini  wakila Sikukuu  ya Krismasi .

Inadaiwa siku iliyofutia  Krismas   majirani  wa  wanadoa  hao  walianza kusikia harumu  mbaya  ikitokea  ndani  ya  nyumba ya  wanandoa  hao  ndipo  walipolazimika  kuvunja   mlango  wa  nyumba  hiyo  na kushuhudia  mwili wa marehemu  ukiwa  umegalagala   sakafuni    chumbani  kwa   wanandoa hao ukiwa na majeraha makubwa  shingoni ,  mgongoni  na  kichwani .

 “Baada ya msako  mkali wa polisi  kwa kushirikiana na  wananchi  mtuhumiwa  alikamatwa  akiwa  anatoroka kwa usafiri wa basi wilayani Sikonge katika mkoa  wa  jirani  wa Tabora……..  baada ya mahojiano  na  polisi  alikiri  kutenda uhalifu  huo ambapo  alimtaja  Ngusa  kuwa  alishirikiana nae “  alidai Kamanda  wa Polisi .

Kidavashari  alionngeza kuwa  mshtakiwa mwingine  Ngusa  alikamatwa  akiwa  anaendelea   na shuguli  zake  kama kawaida  katika Kitongoji  hicho  hca Tulieni  ambapo  wote wawili  wanatarajiwa  kufikishwa mahakamani  mara tu  baada ya  uchunguzi  wa awali wa shauri  hiyo  kukamilika .

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa