Na walter
Mguluchma
Mpanda,Katavi
MKAZI wa kitongoji cha Tulieni kata ya
Itenka wilayani Mlele, Rehema Lubinza (47) ameuawa
kikatili kwa kucharangwa na mapanga na mumewe
kisha mwili wake kufungiwa ndani ya nyumba
kwa siku tatu.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi , Kamishina Dhahiri Kidavashari amethibitisha kutokea kwa tukio hilo lililotokea siku ya mkesha wa Sikukuu ya Krismasi , Desemba 24 usiku katika kitongoji hicho cha Tulieni wilyani Mlele .
Kidavashari alimtaja mtuhumiwa huyo wa mauaji kuwa Mathis Mashini “Igoka’ (46) mkazi wa kitongoji cha kijiji hicho cha Tulieni ambaye ndie mume wa marehemu ..
Kwa mujibu wa Kamishina Kidavashari alidai kuwa kwa siku kadhaa wanandoa hao walikuwa wakishutumiana ambapo mke alikuwa akimshutumu mumewe kwa kushindwa kumpatia mahitaji muhimu ukiwemo unyumba kwa muda mrefu .
Inadaiwa kuwa baada ya kuoana miaka kadha iliyopita , mke ambaye tayari alikuwa ameshajijengea nyumba ya kuishi alimkaribisha mumewe huyo ambapo walikuwa wakiishi i pamoja katika nyumba hiyo ya mwanamke huyo iliyopo katika kitongoji hicho cha Tulieni.
Kwa mujibu wa Kidavashari , mke alimtaka mumewe huyo atoke nyumbani kwake (Rehema) hapo kwa madai kuwa ameshindwa kumpatia matumizi muhimu ukiwemo unyumba kwa muda mrefu kauli ambazo zilimkasirisha mume huyo ambaye inadaiwa hakuwa tayari kuachana na mkewe huyo .
Inaidaiwa mwanamke huyo alimfukuza mumewe huyo nyumba hapo akisisitiza lazima aondoke ndipo mume huyo akishirikiana na mkazi wa kitongoji hiyo aliyetambuliwa kuwa Ngussa Masengwa (39) walimshambulia mwanamke huyo kwa mapanga akiwa amelala nyumbani kwake hapo na kumjeruhi vibaya sehemu mbalimbali ya mwili wake na kumsababishia umauti kisha waliufungia mwili wa marehemu ndani ya nyumba yake hiyo . .
Kwa mujibu wa Kidavashari Siku ya Desemba 25 majirani baada ya kutowaona wanandoa hao huku nyumba yao ikiwa imefungwa mchana kutwa, waliamua kuwasiliana na Mthias kwa simu yake ya mkononi ambaye aliwaeleza kuwa wako Mpanda mjini wakila Sikukuu ya Krismasi .
Inadaiwa siku iliyofutia Krismas majirani wa wanadoa hao walianza kusikia harumu mbaya ikitokea ndani ya nyumba ya wanandoa hao ndipo walipolazimika kuvunja mlango wa nyumba hiyo na kushuhudia mwili wa marehemu ukiwa umegalagala sakafuni chumbani kwa wanandoa hao ukiwa na majeraha makubwa shingoni , mgongoni na kichwani .
“Baada ya msako mkali wa polisi kwa kushirikiana na wananchi mtuhumiwa alikamatwa akiwa anatoroka kwa usafiri wa basi wilayani Sikonge katika mkoa wa jirani wa Tabora…….. baada ya mahojiano na polisi alikiri kutenda uhalifu huo ambapo alimtaja Ngusa kuwa alishirikiana nae “ alidai Kamanda wa Polisi .
Kidavashari alionngeza kuwa mshtakiwa mwingine Ngusa alikamatwa akiwa anaendelea na shuguli zake kama kawaida katika Kitongoji hicho hca Tulieni ambapo wote wawili wanatarajiwa kufikishwa mahakamani mara tu baada ya uchunguzi wa awali wa shauri hiyo kukamilika .

No comments:
Post a Comment