Na Walter Mguluchuma
Mpanda Katavi
Watu
watano wanaosadikiwa kuwa ni majambazi wakiwa na
silaha bunduki iliyotengenezwa kienyeji ambayo inatumia risasi za
SMG wamevamia kijiji cha Katisunga Tarafa ya Nsimbo Wilaya ya Mlele
Mkoani hapa na kuwapola wananchi zaidi ya shilingi laki saba na simu
za aina mbalimbali
Kwa
mujibu wa Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Katavi Kamishina Dhahiri
Kidavashari tukio hilo lilitokea hapo Desemba 15 majira ya saa mbili
na nusu usiku katika kijiji hicho cha Katisunga
Alisema
siku hiyo ya tukio majambazi hao ambao walikuwa na Bunduki iliyokuwa
imetengenezwa kienyeji ambayo ilikuwa ikitumia risasi za SMG
walifika kijijini hapo na kuwavamia wananchi wa kijiji hicho waliokuwa
wafanyabiashara wa vibanda vya kuuza vocha na kutowa huduma ya
M—pesa baada ya kuwatisha kwa kufyatua risasi hewani
Aliwataja
waliopolwa na majambazi hao kuwa ni Richald Thomas aliyepolwa pesa
tasilimu Tsh 320, 000 na simu tatu za wateja ambao walikuwa
wamezipeleka kuchaji Samwel Tito alipolwa pesa tasilimu Tsh 320,000
na simu za aina mbalimbali za wateja wake
Kamanda
Kidavashari aliwataja watu wengine waliopolwa kuwa
ni Joyce Msomba aliyepolwa pesa Tsh 100,000 na simu moja ya
kichina na Mohamed Mrisho aliyepolwa pesa Tsh 20,000 na kufanya jumla
ya pesa zilizopolwa katika tukio hilo kuwa ni Tsh 740,000 NA Simu zenye
thamani ya Tsh 450,000
Alisema mtu
mmoja aitwaye Justine Mkolwa 21 mkazi wa mtaa wa Makanyagio Wilaya
ya Mpanda dereva wa gari aina ya Totota Hiluxe lenye namba za
usajiri T800 ARN amekamatwa kuhusiana na tukio hilo
Aidha alieleza kuwa upelelezi
wa tukio hilo bado unaendelea ilikuwabaini wale wote waliohusika na
tukio ili waweze kufikishwa kwenye vyombo vya sheria

0 comments:
Post a Comment