Home » » AJALI YA BASI DOGO LAUA 1 NA WENGINE 19 WAJERUHIWA WALAZAWA HOSPITALI‏

AJALI YA BASI DOGO LAUA 1 NA WENGINE 19 WAJERUHIWA WALAZAWA HOSPITALI‏

N a Walter Mguluchuma
Mpanda Katavi
Mtu mmoja  Beritine Batazal 42 Mkazi wa Kijiji  cha Mwese  Wilaya ya Mpanda  amekufa  baada ya  basi dogo alilokuwa akisafiria kupinduka baada ya kuacha njia  na  kusababisha watu wengine  19 kupata majeruhi na  kulazwa  Hospital
Kwa mujibu wa Kamanda wa polisi wa Mkoa wa  Katavi Kamishina Dhahiri Kidavashari  ajari hiyo ilihusisha basi dogo aina ya Hino lenye namba za usajiri  T 894 APW  lililokuwa likiendeshwa  na mmiiliki wa gari hilo Dickson  Kinyonto ambae alitoroka baada ya kutokea tukio
Kidavashari  alieleza ajali hiyo ilitokea hapo Desemba 16 majira ya saa sita na nusu mchana  katika eneo la Ilembo  umbali wa kilimeta tatu kutoka Mpanda mjini  barabara  ya Mpanda ya kwenda  Sumbawanga  Mkoa wa Rukwa
Alisema gari hilo ambalolilikuwa litikokea  Tarafa ya Mpimbwe Wilaya ya Mlele  likielekea Mpanda  mjini lilipata ajali hiyo baada ya taili lambele la upande wa kushoto kupasuka  na ndipo lilipoacha njia  na kupinduka na kusababisha kifo cha  Beritine na majeruhi 19 ambao wamelazwa katika Hospitali ya wilaya ya Mpanda na watatu kati yao hari zao sio nzuri
Kamanda Kidavashari aliwataja majeruhi hao kuwa ni Charles Sokoni  25 mkazi wa mtaa wa Nsemlwa mjini Mpanda ,George  Sengeka  48 mkazi wa  Mpimbwe, January Damiano  38 mkazi wa mtaa wa Kasimba  Ezekiel  Benjamin 44  mkazi wa Kashaulili Mpuluku  Magobo mkazi wa Ikingwa  Saimoni  Bala  25 Mkazi wa kata ya Kibaoni
Majeruhi wengine ni  Paul  Clement 28  mkazi wa kijiji cha  Tinde  Lyoba  Mengo  36 mkazi wa Majimoto  E 3170 CPL  Albano polisi wa kituo cha Kibaoni  Selemani  Njala  62 mkazi wa kijiji cha Sosayati  Magret  Cosmas  29 Usinge   Justine  Michael  17 Bariadi Shinyanga , Cristina  Gabriel 60  Stalike Mlele , na Kabura  Sahani Majimoto Mpimbwe
Kidavashari alisema majeruhi  wote wanaendelea kupatiwa matibabu kwenye Hospitali ya Wilaya ya Mpanda  na mwili wa marehemu  Beritine  wamekabidhiwa ndugu zake   kwa ajali ya mazishi yatakayo fanyika kesho kijijini kwao mwese 
Jeshi la polisi linaendelea  kumtafuta  mtumiwa  dereva wa gari hilo  Dickson Kinyonto  ambae alitoroka  baada ya Tukio ili aweze kufukishwa mahakamani kujibu tuhuma za  kusababisha ajali

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa