Home » » WAWILI WAFA KATIKA AJALI YA PIKIPIKI KATIKA MATUKIO MAWILI TOFAUTI‏

WAWILI WAFA KATIKA AJALI YA PIKIPIKI KATIKA MATUKIO MAWILI TOFAUTI‏

N a Walter Mguluchuma-katavi yetu Blog
Mpanda Katavi
Watu wawili wamekufa wilayani Mpanda Mkoa wa Katavi katika matukio mawili tofauti ya ajali ya pikipiki likiwemo la mwanafunzi mmoja kugongwa na pikipiki na kufa hapo hapo wakati akitokea shuleni wakati akiendesha Baiskeli
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashari tukio la kwanza la mwanafunzi wa shule ya msingi Mbungani Bundala  Shija (12) kugogongwa na pikipiki na kufa hapo hapo lilitokea hapo  juzi majira ya saa kumi na mbili na nusu asubuhi
Alisema siku hiyo Bundala alikuwa ametoka nyumbani kwao akiwaanaelekea shuleni  ya msingi Mbugani Kata ya Kakese alikuko kuwa anasoma huku akiendesha baiskeli ndipoalipogongwa na pikipiki  yenye namba  T937 CFF aina ya TOYO iliyokuwa ikiendeshwa  na Kasansa  Protas (25) mkazi wa Kijijicha Kakese Mbugani Wilayani hapa
Alieleza mbali ya mwanafunzi huyo kufa hapo hapo dreva wa Pikipiki nae aliumia vibaya  kutokana na ajari hiyo na amelazwa katika hospitali ya Wilaya ya Mpanda akiendelea kupatiwa matibabu huku akiwa chini ya ulunzi wa Polisi
Katika tukio la pili mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la  Geofrey  Anatory Vicent  40  mkazi wa Mtaa wa Mpanda Hotel amefariki dunia baada ya kudondoka kwenye pikipiki ambayo alikuwa amebebwa
Kamanda Kidavashari alisema tukio hilo lilitokea hapo Novemba 10 mwaka huu katika eneo la mtaa  Nsemlwa kichangani mjini hapa majira ya saa tano na nusu asubuhi
Alisema siku hiyo ya tukio marehemu alikuwa amepanda pikipik yenye namba za usajiri  T372 AXE iliyokuwa ikiendeshwa  na  Armoury Seif Esry 32 mkazi wa  mtaa wa Madukani mjini hapa na baada ya kudondoka alifariki dunia hapo hapo
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi amewaonya waendesha vyombo vya moto wasio zingatia  sheria na taratibu  za usalama Barabarani kuwa hatua kali za kisheria  zitachukuliwa dhidi  yao  ili kunusuru  watu  wasiendelee  kuathilika  na uzembe huo

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa