N a Walter
Mguluchuma-Katavi yetu Blog
Mpanda Katavi
Watu
wasiofahamika wamesalimisha silaha Bunduki
aina ya Sub Machine Gun katika kijiji cha Inyonga Wilaya ya Mlele
Mkoa wa Katavi ikiwa na magazini moja ambayo haikuwa na risasi nyumbani kwa
Afisa Mtendaji wa Kijiji hicho cha Inyonga Abiud Vilima
Kamanda wa Polisi
wa Mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashari alisema tukio hilo la kusalimisha silaha
lilitokea hapo jana majira ya kumi na mbili asubuhi nyumbani kwaafisa mtendaji
huyo
Alisema siku
hiyo watu wasiofahamika walisalimisha
Bunduki hiyo usiku nyumbani kwa Abiud
wakati yeye na familia yake wakiwa wamelala usingizi ndani ya nyuma yao
pasipo kujua
Kidavashari
alieleza ndipo ilipotimia majira ya saa kumi na mbili Asubuhi majirani wa
mwenyekiti huyo wa kijiji wakati wakiwa wanaelekea kwenye shughuli zao za
maandalizi ya kilimo ndipo walipo iona Bunduki hiyo ikiwa imetelekezwa nyumbani
kwa Afisa mtendaji wao wa Kijiji
Alisema ndipo
walipomwamsha afisa huyo mtendaji ambae nae alishikwa na mshangao kuona silaha
hiyo ikiwa imetelekezwa nyumbani kwake
hari ambayo ilimlazimu atowe taarifa kituo cha plisi cha Wilaya ya Mlele
ambao walifika muda si mrefu na kuichukua silaha hiyo
Kidavashari
alifafanua kuwa mafanikio hayo ya usalimishaji wa silaha huo umeyokana na
elimu ya polisi jamii inayoendelea
kutolewa na jeshi la polisi kwa wananchi
katika maeneo mbalimbali hapa nchini
Pamoja na hofu ya
wananchi juuya operesheni zinazoendelea hapa nchini kama vile Okoa maliasili na
jeshi la polisi mkoa wa Katavi linaendelea na uchunguzi wa kuwabaini watu wanao
miliki silaha kihalali na wanazitumia silaha zao kinyume na umilikaji wa vibari
vyaoili waweze kuchukuliwa sheria dhidi yao
KAMA KUNA GAZETI LINAHITAJI KUTUMIA HABARI HII WASILIANA NASI KWA NAMBA 0654221465

0 comments:
Post a Comment