Home » » WACHIMBAJI WA MADINI WAPEWA MAFUNZO YA KULIPUA MIAMBA KWA KUTUMIA BARUTI‏

WACHIMBAJI WA MADINI WAPEWA MAFUNZO YA KULIPUA MIAMBA KWA KUTUMIA BARUTI‏


 Wachimbaji wa madini wa mkoa wa katavi wakiwa kwenye mafunzo ya siku nne yaliyoandaliwa na taasisi ya mizinga ya mkoani morogoro iliyochini ya jeshi la ulinzi la kujenga taifa wakifundishwa namna ya kulipua mashimo ya miamba ya madini kwa kutumia baruti mafunzo haya yanafanyika katika ukumbi wa super city mjini mpanda.
picha na walter mguluchuma

Meneja wa taasisi ya mizinga yenye makao makuu yake mjini morogoro taasisi inayosimamiwa na jeshi la ulinzi la kujenga taifa PINGU KAMENYI  akifungua mafunzo ya siku nne ya wachimbaji wa madini wa mkoa wa katavi mafunzo hayo yenye lengo la kuwafundisha namna ya kulipua mashimo ya miamba kwa kutumia baruti 
picha na walter mguluchuma-Katavi yetu Blog

N a Waltel   Mguluchuma
Mpanda Katavi yetu blog
 Taasisi ya Serikali  ya Mzinga yenye makao yake Morogoro  inayosimamiwa  na Wizara  ya ulinzi na jeshi la kujenga Taifa  inaendesha mafunzo kwa washimbaji wa  madini  wa Mkoa wa Katavi (KARAMA) huu ya namna ya kulipua miamba ya madini kwenye mashimo kwa kutumia  Baruti

Mafunzo hayo ya siku nne yalifunguliwa hapo jana  kwenye ukumbi wa Super City uliopo mjini hapa na meneja wa mauzo  wa Tasisi ya Mzinga  bwana Pingu Kamenyi

Alisema  wachimbaji wengi wanaochimba  madini  hapa nchini  wamekuwa sio wachimbaji rasmi wa madini  kutokana  na kufanya kazi nje  ya utarabibu

Hivyo  mafunzo hayo yatawapa uwezo wa kufanya shughuli hizo kwa utaalamu hari itakayo wafanya waongeze pia kipato chao  kwa hari hiyo mafunzo yatawaongezea uwezo

Aliwataka wachimbaji kuacha tabia ya kuajiri watu waliochini ya miaka kumi na  nane kwenye migogi yao kwani  ni sheria  inakaza watu chini ya umri huo kufanya kazi kwenye maeneo yote yanayojishughulisha na shughuli za uchimbaji wa madini

Kamenyi aliwaeleza kuwa taasisi ya Mzinga kwa kutambua umuhimu wa wachimbaji  wa Mkoa wa Katavi imeamua kujenga ofisi zake  katika eneo la Misunkumilo ili kuwapunguzia  gharama wachimbaji za  ununuaji wa baruti kwani ofisi hiyo itakapofunguliwa watauziwa  kwa bei ya chini  kuliko ilivyo sasa ambapo wanalazimika kwenda kununua nje ya mkoa wa Katavi

Kwa upande wake  mhandisi  migodi  wa kanda ya  magharibi  Giruad  Luyoka aliwaeleza kuwa  mafunzo hayo  yatawasaidia  pia kupunguza vifo vilivyokuwa vikitokea wakati wa ulipuaji wa  miamba kwa kutumia baruti

Alifafanua kuwa wako baadhi ya wachimbaji wamepoteza maisha kutokana  na kutoelewa wasimame wapi  wakati wanalipua  mashimo ya miamba  hivyo mafunzo haya  yatawawezesha wajue  mahari pakusimama kwenye maeneo ya usalama
Nae mmoja wa washimbaji   hao Andrea Ikololo  alieleza kuwa  wachimbaji wengi walikuwa wakipata madini kidogo kutokana na kutofahamu utaalamu  wa kulipua  mashimo ya miamba kwa kutumia baruti  hivyo mafunzo hayo yatawaongezea utaalamu  kuliko walivyokuwa mwanzo

Katibu wa wachimbaji wa madini wa Mkoa wa Katavi  (KATAREMA)   Joji Kasanda   alisema  wachimbaji  wamethamini sana mafunzo hayo na ndio maana idadi yao imeongezeka kutoka  idadi iliyokuwa imepangwa ya washiriki 30 hadi wamefikia 65

Mafunzo hayo yamewashirikisha washimbaji mbalimbali wa aina za madini yanayopatikana katika Mkoa wa Katavi  kama Vile dhahabu,shaba  ulunga na mengineyo




0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa